• HABARI MPYA

    Thursday, September 04, 2014

    PASHA PASHA LIGI KUU BARA; COASTAL UNION YAWAFUMUA 10-0 MABINGWA WA ZANZIBAR

    Na Mwandishi Wetu, PEMBA
    MSHAMBULAJI mpya wa Coastal Union aliyesajiliwa kutoka Gor Mahia ya Ligi Kuu ya Kenya, Itubu Imbem raia wa Kongo, ameanza kuonesha cheche zake baada ya kuifungia timu hiyo mabao matatu katika mechi yao kirafiki waliyoshinda 10-0 dhidi ya Falcon FC ya Pemba kwenye Uwanja wa Gombani, Pemba jana.
    Falcon FC, iliyowahi kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya Zanzibar, inashiriki Ligi Daraja la Kwanza visiwani humo baada ya kuteremka daraja na juzi ilikumbwa na dhahama hiyo ya mabao kutoka kwa mabingwa wa Tanzania Bara 1988 waliosajili wachezaji wengi wapya baada ya kikosi chao kufanya vibaya msimu uliopita huku kukitokea mgogoro wa kiuongozi.
    Itubu Imbem kushoto wakati anasaini Coastal Union

    Coastal Union walioonekana kujiamini na kujipanga vilivyo, walilishambulia kwa fujo lango la Falcon na kupata magoli hayo, wakipata magoli matano katika kila kipindi.
    Magoli ya mengine Coastal Union yalifungwa na Abasi Athumani ambaye alipachika matatu pia (Hat-Trick) wakati Mahundi Petro na Mbwana Hamisi kila mmoja akipachika goli moja.
    Mchezaji mwingine aliyesajiliwa kutoka Gor Mahia, Mkenya Rama Salim naye  alitikisa nyavu mara mbili na kuhitimisha karamu ya magoli kwa Coastal inayonolewa na Yusuph
    Chippo alisema kuwa kutokana na maandalizi waliyoyafanya wakiwa visiwani humo wanamatumaini makubwa ya kufanya vizuri katika michuano ya Ligi kuu soka Tanzania bara itakayoanza Septemba 20 mwaka huu.
    “Sasa kikosi changu kimeimarika kwani juzi tuliifunga Opec ya kisiwani hapa mabao 11-0, hivyo kikosi changu kipo tayari kushiriki Ligi Kuu tukianzia na mechi yetu dhidi ya Simba kwa kuchukua pointi tatu muhimu," alisema Chippo baada ya mechi hiyo.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: PASHA PASHA LIGI KUU BARA; COASTAL UNION YAWAFUMUA 10-0 MABINGWA WA ZANZIBAR Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top