• HABARI MPYA

    Friday, September 26, 2014

    WENGER AWAANZISHIA TENA MAN CITY NA USAJILI WAO WA KIMAGUMASHI KWA FRANK LAMPARD

    MPANGO wowote wa kuongeza muda wa Frank Lampard kuendelea kucheza kwa mkopo Manchester City unaweza kuibua maswali zaidi ya kimaadili juu ya uhamisho wake, kwa mujibu wa kocha Arsenal, Arsene Wenger.
    Lampard alisaini timu ya Ligi Kuu ya Marekani (MLS), New York City baada ya kutemwa Chelsea, kabla ya kurejea ghafla Ligi Kuu ya England kujiunga na mabingwa, ambao pamoja na kuinunua timu ya baseball ya nchini humo, wakanunua na hisa timu hiyo ya MLS.
    Kiwango kizuri cha mkongwe huyo mwenye umri wa miaka 36, aliyefunga mabao mawili katika ushindi wa 7-0 Kombe la Ligi, maarufu kama Capital One Cup dhidi ya Sheffield Jumatano, kimeibua tetesi kwamba City itaangalia uwezekano wa kumbakiza ifikapo Januari.

    Frank Lampard alijiunga na Man City kwa mkopo wa muda mfupi baada ya kuondoka Chelsea msimu huu

    Msimu wa MLS 2015 unatarajiwa kuanza tena Machi, mwakani na Lampard amesema hajafanya majadiliano yoyote na City juu ya mustakabali wake mwishoni mwa mwaka.
    Wenger, ambaye alimrudisha kwa mkopo Nahodha wake wa zamani The Gunners, Thierry Henry kutoka New York Red Bulls Januari 2012, anaamini namna yoyote ya kuongeza mkataba wa mkopo wa Lampard kwa sasa haitakuwa nzuri, hata ikiwa ni ndani ya utaratibu wa Ligi Kuu.
    "Wakati wote una maamuzi ya aina mbili, moja ya kimaadili na pili ni ya kisheria na ni juu ya unavyochukulia,"amesema Wenger.
    "Nafikiri, hii ni sheria? lazima uheshimu hilo na kisha mchezaji lazima atazame uamuzi wake. Naheshimu ukweli kwamba anataka kucheza katika kiwango cha juu na labda hakuwa na nafasi zaidi Chelsea. Sijui haswa kilicho nyuma ya hili,".
    "Ulikuwa ni mpango wake kwenda New York na kwenda Man City? Sina uhakika. Nafikiri kabisa alitaka kwenda nje na kutua New York, na (kisha) kupewa ofa ya kurudi Ligi Kuu England na kuichukua. Anaweza kufafanua vizuri yeye mwenyewe kuliko ninavyofanya, sijui nini kipo nyuma ya hili,"amesema Wenger.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: WENGER AWAANZISHIA TENA MAN CITY NA USAJILI WAO WA KIMAGUMASHI KWA FRANK LAMPARD Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top