• HABARI MPYA

    Sunday, September 21, 2014

    FALCAO AKIUMIA TU, MKATABA WAKE UNAVUNJWA MAN UNITED

    KLABU ya Manchester United inaweza kumrudisha Radamel Falcao katika klabu yake, Monaco iwapo ataumia goti lililomfanya awe nje ya Uwanja kwa muda mrefu msimu uliopita.
    Mshambuliaji huyo Colombia amehamia Old Trafford kwa mkopo wa Pauni Milioni 6 mwaka mmoja akikamilisha uhamisho wake siku ya mwisho na analipwa wastani wa Pauni 300,000 kwa wiki. 
    Lakini United katika kuhakikisha uwezekezaji huo hauwi wa hasara, katika Mkataba wao wakaweka kipengele cha kumrudisha iwapo ataumia tena.

    Radamel Falcao alicheza kwa dakika 20 dhidi ya QPR, akitokea benchi katika mechi yake yake ya kwanza Manchester United
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: FALCAO AKIUMIA TU, MKATABA WAKE UNAVUNJWA MAN UNITED Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top