• HABARI MPYA

    Thursday, September 04, 2014

    ROONEY AITENDEA HAKI BEJI YA UNAHODHA ENGLAND, APIGA BAO LA USHINDI THREE LIONS WAKING'ATA MTU WEMBLEY

    NAHODHA wa England, Wayne Rooney ameitendea haki beji katika mchezo wake wa kwanza tangu arithi mikoba ya Steven Gerrard aliyestaafu, baada ya kufunga bao pekee katika ushindi wa 1-0 dhidi ya Norway Uwanja wa Wembley usiku huu.
    Nahodha huyo wa Manchester United pia, alifunga bao hilo pekee kwa mkwaju wa penalti dakika ya 68, kufuatia nyota wa Liverpool, Raheem Sterling kuchezewa rafu kwenye eneo la penalti.
    Katika mchezo huo uliohudhuriwa na watu 40,181 – idadi ndogo zaidi ya mahudhurio kwenye Uwanja wa Wembley tangu ufunguliwe tena, kinda Sterling alizawadiwa heshima ya mchezaji bora mechi baada ya kazi nzuri kwenye kikosi cha Roy Hodgson usiku huu.
    Nahodha babu kubwa; Wayne Rooney akipongezwa na wenzake baada ya kufunga bao pekee usiku huu
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: ROONEY AITENDEA HAKI BEJI YA UNAHODHA ENGLAND, APIGA BAO LA USHINDI THREE LIONS WAKING'ATA MTU WEMBLEY Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top