• HABARI MPYA

    Thursday, September 04, 2014

    MIROSLAV KLOSE, PHILIPP LAHM NA MERTESACKER WAPEWA TUZO ZA HESHIMA UJERUMANI

    WAKONGWE Miroslav Klose, Philipp Lahm na Per Mertesacker wamepewa tuzo za heshima usiku huu kabla ya mchezo wa kirafiki kati ya Ujerumani na Argentina Uwanja wa Esprit Arena.
    Watatu hao waliichezea Ujerumani katika fainali ya Kombe la Dunia mwaka 2014 dhidi ya Argentina kabla ya kuamua kustaafu soka ya kimataifa.
    Klose, ambaye ni mfungaji bora wa kihistoria wa Ujerumani kwa mabao yake 71, ametungika daluga baada ya kuwa mfungaji wa mabao mengi zaidi katika historia ya Kombe la Dunia.
    Heshima: Per Mertesacker, Miroslav Klose na Philipp Lahm baada ya kukabidhiwa tuzo zao Esprit Arena

    MCHANGO WAO KATIKA TIMU YA TAIFA UJERUMANI...

    Miroslav Klose (Lazio) - Mechi 137, mabao 71 
    Philipp Lahm (Bayern Munich) - Mechi 113, mabao 5
    Per Mertesacker (Arsenal) - Mechi 104, mabao 4
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MIROSLAV KLOSE, PHILIPP LAHM NA MERTESACKER WAPEWA TUZO ZA HESHIMA UJERUMANI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top