• HABARI MPYA

    Thursday, September 04, 2014

    MARCOS ROJO APATIWA KIBALI CHA KUPIGA MZIGO MAN UNITED, VAN GAAL SASA ROHO KWATUUU

    BEKI mpya wa Manchester United, Marcos Rojo anaweza kuichezea kwa mara ya kwanza klabu yake hiyo katika mchezo wa Ligi Kuu ya England dhidi ya Queens Park Rangers Uwanja wa Old Trafford Septemba 14 baada ya kupatiwa hati ya kufanya kazi.
    Rojo alisafiri hadi Lisbon Alhamisi ili kukamilisha taratibu za kupata hati hiyo ya kufanyia kazi England.
    Kufanikiwa kwa mchezaji huyo kupata hati hiyo ya kufanyia kazi ni faraja kwa kocha Louis van Gaal, ambaye kikosi chake mina tatizo la safu ya ulinzi.

    Uthibitisho: Marcos Rojo amepatiwa hati ya kufanyia kazi maana yake sasa anaweza kuichezea Manchester United kwa mara ya kwanza dhidi ya QPR

    Taarifa ya Manchester United kwenye ukurasa wake wa Twiter 
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MARCOS ROJO APATIWA KIBALI CHA KUPIGA MZIGO MAN UNITED, VAN GAAL SASA ROHO KWATUUU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top