• HABARI MPYA

    Friday, September 19, 2014

    EVERTON YAANZA VYEMA EUROPA LEAGUE, YAWAFUMUA WAJERUMANI 4-1

    KLABU ya Everton ya England imeanza vyema michuano ya Europa League baada ya kuichapa Wolfsburg ya Ujerumani manbao 4-1 Uwanja wa Goodison Park.
    Kikosi cha Roberto Martinez kilionyesha ni moto tangu mapema tu kwenye mchezo huo, baada ya
    Ricardo Rodriguez kujifunga mapema tu akijaribu kuokoa shuti la Steven Naismith kuipatia Everton bao la kuongoza. 
    Seamus Coleman akafunga la pili karibu na mapumziko na Leighton Baines aliyechangia mabai yote ya awali, akafunga la tatu kwa penalti baada ya Aiden McGeady kuchezewa faulo. 

    Kevin Mirallas akafunga bao la nne dakika za mwishoni kabla ya Rodriguez kuwafungia wageni bao la kufutia machozi kwa mpira wa adhabu wa dakika ya mwisho.
    Kikosi cha Everton kilikuwa; Howard, Coleman/Osman dk90, Stones, Jagielka, Baines, Barry, McCarthy, McGeady, Naismith/Gibson dk82, Mirallas na Lukaku/Eto’o dk69. 
    Wolfsburg: Benaglio, Jung, Knoche, Naldo, Rodriguez, Luiz Gustavo/Guilavogui dk77, Malanda/Hunt dk46, De Bruyne, Arnold, Caligiuri/Bendtner dk60 na Olic.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: EVERTON YAANZA VYEMA EUROPA LEAGUE, YAWAFUMUA WAJERUMANI 4-1 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top