// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); SIMBA WAGOMA MAZUNGUMZO NA AZAM - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE SIMBA WAGOMA MAZUNGUMZO NA AZAM - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Sunday, December 09, 2012

    SIMBA WAGOMA MAZUNGUMZO NA AZAM

    Kaburu kushoto wakati anamkabidhi jezi Ngassa baada ya kusaini kwa mkopo Simba

    Na Mahmoud Zubeiry
    MAKAMU Mwenyekiti wa Simba SC, Geoffrey Nyange ‘Kaburu’ amesema klabu yake haiku tayari kufanya mazungumzo na Azam FC, kuhusu suala la kuuzwa kwa mchezaji Mrisho Ngassa katika klabu ya El Merreikh ya Sudan, kwa sababu hawatendewi uungwana na klabu hiyo.
    Kaburu ameiambia BIN ZUBEIRY jana kwamba, klabu yake iliingia mkataba na Azam FC kwa kununua haki zote za huduma za Ngassa kwa mwaka mmoja, hadi Mei 21 mwakani, ikilipa Sh. Milioni 25 kama ada ya kumtumia mchezaji huyo kwa mwaka mmoja pamoja na kumlipa mchezaji haki zake zote stahiki za kimkataba ikiwemo mshahara wake.
    Kaburu amesema Azam bila ya kuzingatia mkataba iliousaini na Simba SC, na matakwa ya FIFA yanayohusu mkopo, iliamua kutangaza kumuuza Ngassa bila ya kuihusisha Simba wakati ikijua kuwa ilikuwa na Mkataba na Simba SC ambayo ameishaichezea katika mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu ya Bara.
    “Kitendo cha Azam FC kuongea na Klabu ya El Merreikh FC na kuweka makubaliano ya mauzo ya mchezaji na kumtangaza kuwa kimemuuza mchezaji Ngassa bila ya kuihusisha Simba SC, na baadaye kuiandikia klabu ya Simba kuwa kimeamua kumrudisha mchezaji Ngassa Azam, wakati ikijua kuwa ina mkataba na Simba SC ni uvunjifu mkubwa wa taratibu na umeleta athari kubwa kwenye klabu yetu,”alisema Kaburu na kuongeza;
    “Tayari Simba SC ilikwishatuma malalamiko TFF na kupeleka pingamizi lake juu ya sulala hili kwa Rais wa TFF, Leodegar Tenga, ambapo imeamuliwa kuwa suala hili liende kwenye Kamati ya Sheria, Katiba na Hadhi ya Wachezaji likapatiwe ufumbuzi,”alisema.
    Amesema Simba imekuwa ni klabu yenye kuangalia zaidi maslahi ya wachezaji na haina kipingamizi kwa kuwaruhusu wachezaji wake kutoka pindi wanapopata timu nje ya nchi kama utaratibu unafuatwa.
    Kaburu amesema Simba SC ilikuwa tayari kukaa mezani na Azam kwa mazungumzo, lakini kwa kuwa Azam haipo tayari kutambua haki za Simba SC na imekuwa ikilitekeleza suala hili kiholela, hivyo haioni sababu za kuzungumza na Azam FC na kuliacha suala hili liende kwenye Kamati ya Sheria, Katiba na Hadhi ya Wachezaji kama TFF ilivyoagiza.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments
    Item Reviewed: SIMBA WAGOMA MAZUNGUMZO NA AZAM Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top