• HABARI MPYA

    Saturday, May 19, 2012

    CECH AJIANDAA KWA PENALTI


    EPL:Petr Cech, Chelsea v Newcastle United
    Getty
    KIPA wa ChelseaPetr Cech amekuwa akifanya mazoezi ya kuokoa mikwaju ya penalti kama tahadhari iwapo fainali ya Ligi ya Mabingwa leo itaamuliwa kwa mapigo hayo.

    Kipa huyo mwenye umri wa miaka 29 alicheza fainali ya mwaka 2008, wakati The Blues walipofungwa kwa mikwaju ya penalti Manchester United kufuatia sare ya 1-1.

    Na ingawa anajiamini kikosi cha Roberto Di Matteo kina uwezo wa kushinda ndani ya muda wa kawaidea Uwanja wa Allianz Arena, Cech amesema kwamba amekuwa akiangalia hatua za wachezaji wa Bayern walipokuwa wanapiga penalti katika mechi za awali na sasa anajua vema namna ya kuwaokolea penalti zao.

    Kipa huyo aliyesajiliwa kwa dau la pauni Milioni 7, akitokea Rennes ya Ufaransa  mwaka 2004, Cech kesho anafikisha miaka 30 na amesema angependa kusherehekea kuzaliwa kwake sambamba na taji la ubingwa wa Ligi ya Mabingwa Magharibi mwa London.  “Kama nitapata Kombe, sitahitaji keki,” alisema.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: CECH AJIANDAA KWA PENALTI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top