• HABARI MPYA

    Saturday, May 12, 2012

    TWIGA STARS YAPIGWA 'ARBAA' NYUMBANI


    Kocha wa twiga, Charles Boniface Mkwasa akishuhudia mvua ya mabao

    TIMU ya taifa ya soka ya wanawake ya Tanzania, Twiga Stars kwa ‘bakhti mbaya’ leo imechapwa mabao 4-1 katika mchezo wa kimataifa wa kirafiki uliofanyika kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
    Mchezo huo ulikuwa ni hamususi kwa kuzinoa timu hizo zinazojiwinda na mechi zake za kuwania kucheza fainali za Afrika kwa Wanawake (AWC) ambazo Twiga itakwaana na Etthiopia Mei 26 mwaha huu huku Zimbabwe itakipiga na Nigeria.
    Kipigo cha Twiga dhidi ya  Zimbabwe ni mara ya pili  ambapo mara ya kwanza ilikuwa nusu fainali ya Kombe la COSAFA ambapo katika mechi hiyo iliyochezwa Julai 5 jijini Harare , Zimbabwe ilishinda kwa penalti 4-2.
    Aidha, timu ambazo jana ilikuwa mara ya tatu kukutana, mara ya pili walkikwaana kwenye michezo ya All Africa Games (AAG) iliyofanyika Maputo , Msumbiji ambapo timu hizo zilitoka sare ya mabao 2-2.
    Katika mchezo wa jana, Rufaro Machungura aliiandikia Zimbabwe bao la kwanza katika dakika ya 5 ya mchezo baada ya mabeki wa Twiga kujichanganya.
    Dakika ya 17 Nokuthula Ndolovu alimalizika kazi nzxuri ya washambuliai wake kwenye eneo la hatari  na kuandika bao la la pili ambalo lilidumu hadi timu hizo zinakwenda mapumziko ambapo Zimbabwe ilikuwa ikiongoza mabao 2-0.
    Kipindi cha pili kilianza kwa timu zote kucheza kwa taratibu kabla ya Asha Rashid kuiandikia Twiga bao lake pekee katika dakika ya 46 akimalizia kazi nzuri ya Mwanahamis Omari.
    Zimbabwe ilitikisa nyavu za Twiga kwa mara ya tatu katika dakika ya 54 kupitia kwa Nokuthula alipotumia vema uzembe wa beki wa Twiga Fatma Khatib aliyerkuwa katika harakati za kuokoa krosi yake.
    Rufaro Machungura alifunga karamu ya mabao kwa Zimbabwe katika dakika ya 74 ambalo lililidumu hadi dakika 90 ya mchezo huo iliyomalizika kwa Zimbambwe kushinda 4-1.
    Aidha, mchezo huo ambao ulichelewa kupigwa kutoka na mvua iliyonyesha jana jijini Dar es Salaam, Mwamuzi wa kimataifa JudithhGamba alimzawadia kadi ya njano nyota wa Twiga  Fatma Bashir kwa kumchezea vibaya Rufaro.
    Katika mchezo huo Twiga ilifanya mabadiliko na kuwatoa Rukia Khamis, , Zena Khamis , Mwajuma Abdallah,na Fatma Hatib na kuwaingiza  kuwaingiza Fadhila Hamadi,  Amina Ally, Siajab Hassan na Mwanaid Tamba. 
    Baada ya mchezo huo Twiga ambayo ilipata nafasi nyingi za wazi na kushindwa kuzitumia walidai  kufungwa kwao kulichangiwa na mvua.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: TWIGA STARS YAPIGWA 'ARBAA' NYUMBANI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top