| Zizou na Keane enzi hizo babake, watoto wa jana mbona mlikosa raha jamani! |
03/05/2012 12:50,
Reds legends to play in Madrid
WACHEZAJI wa zamani wa wa Manchester United na Real Madrid watamenyana mwezi ujao katika mechi ya hisani, iliyoandaliwa na mabingwa hao wapya wa Hispania.
Magwiji wa klabu zote wameorodheshwa kwa ajili ya mechi hiyo iitwayo Corazon Classic Match 2012, inayotarajiwa kufanyika kwenye Uwanja wa Santiago Bernabeu Jumapili ya Juni 3, mwaka huu.
Mechi ya marudiano itafanyika kwenye Uwanja wa Old Trafford na imekubaliwa ichezwe mwakani, Juni 2, 2013.
Wachezaji wa Mashetani Wekundu wanaotarajiwa kuwamo ni pamoja na Roy Keane, Edwin van der Sar, Denis Irwin, Andy Cole, Dwight Yorke na Bryan Robson wakati upande wa Real Madrid ni Zidane, Figo, Redondo, Hierro,Butragueño, Sanchís, Helguera na Morientes. Kwa baadhi ya wachezaji itakuwa ni mechi ya marudiano - kwani United na Real Madrid zilikutana katika Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa mwaka 2000 na 2003 na vigogo wa Hispania wakashinda mechi zote, 3-2 na 6-5 kwa matokeo ya jumla.
Lengo la mechi hii ni kusapoti mradi wa hisani wa Real, Real Madrid Foundation Afrika na tiketi zitauzwa kwa euro 10 na 15 kwa mtandao wa www.realmadrid.com/fundacion.
Taarifa zaidi kuhusu mechi ya marudiano mwakani Old Trafford - kusapoti mradi wa Man U, Manchester United Foundation - zitatolewa baadaye.


.png)
0 comments:
Post a Comment