• HABARI MPYA

    Saturday, May 19, 2012

    PIRATES WATWAA UBINGWA AFRIKA KUSINI


    Football | Absa Premiership

    Siyabonga Sangweni © Backpagepix

    Benni Mc Carthy ang'ara akipiga mabao mawili



    KLABU ya Orlando Pirates jioni hii imetetea ubingwa wa Afrika Kusini, hilo likiwa taji lao la sita ndani ya misimu miwili wakishinda mabao 4-2 dhidi ya Golden Arrows mjini Durban.
    Katika mchezo huo, Benni McCarthy alifunga mabao mawili katika dakika za 60 na 90, wakati mabao mengine ya Pirates yalifungwa na Legwathi dakika ya 25 na Siyabonga Sangweni dakika ya 30.

    Moroka Swallows, timu pekee iliyobakia kwenye mbio za ubingwa kuelekea mechi za mwisho leo, iliifunga Maritzburg United 1-0.
    Santos itacheza mechi maalum ya kuwania kujinusuru kushuka daraja licha ya ushindi wa 1-0 dhidi ya Jomo Cosmos.
    Black Leopards iliifunga Ajax Cape Town mabao 3-1 na kufanikiwa kubaki Ligi Kuu.

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: PIRATES WATWAA UBINGWA AFRIKA KUSINI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top