| Hapa ni baada ya Tegete kuifunga Simba kwa mara ya kwanza Aprili 19, mwaka 2009 |
KUPANDA na kushuka kwa kiwango cha mwanasoka ni kawaida na
wengi wamepitia hali hiyo- Jerry Tegete akiwa miongoni mwao.
Huu ni msimu wa pili, Tegete amezimika, akiwa hatambi Yanga
na hana nafasi hata timu ya taifa japo ya Bara, Kilimanjaro Stars.
Vigumu kujua sababu za kushuka kwa kiwango cha Tegete,
lakini ukitulia na kufuatilia matukio yake ya siku za karibuni unaweza kubaini
sababu.
Mkanganyiko wa mawazo- kitaalamu frustrations ndio kwa kiasi
kikubwa ilimuondoa mchezoni Tegete.
Itakumbukwa hadi misimu miwili iliyopita, Tegete alikuwa
mchezaji wa timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars na chaguo la kwanza kwenye
klabu yake, Yanga tena akiwa kipenzi cha wapenzi wa soka kuanzia klabu hadi
taifa.
Lakini ghafla mambo yakaanza kumbadilikia kuanzia Yanga, ambako
mashabiki walianza kumuona hafai wakidai anakosa sana mabao na timu ya taifa
akatemwa. Tegete alidhani labda kocha Mganda Sam Timbe alikuwa adui wa kipaji
chake, lakini hata baada ya kurejea Kostadin Papic, hakuna tofauti.
Awali, aliona kama anaonewa na akaanza kukata tamaa na hiyo
ikachangia zaidi kushusha kiwango chake, lakini baada ya kujiridhisha kiwango
chake kweli kimeshuka, Jerry alibadilika.
| Tegete akiwainua mashabiki wa Yanga katika Kombe la Tusker mwaka 2009, Uwanja wa Uhuru |
Tangu mwanzoni mwa mwaka huu, Tegete amekuwa katika jitihada
nzito za mazoezi hali ambayo kwa sasa inawaridhisha hadi makocha wake, hususan
Kocha Msaidizi Fred Felix Minziro, ambaye kwa sasa anaiongoza timu wakati Papic
amewekwa kando.
Ni namna gani Tegete atawashika tena wapenzi wa Yanga? Ni jinsi
gani Tegete atarudisha heshima yake katika soka ya Tanzania- ili kujitengenezea
mazingira ya kurejeshwa timu ya taifa?
Jibu ni kuongeza bidii katika mazoezi, ili aanze vema msimu ujao.
Anaikosa mechi ya Mei 5, 2012- yaani Jumamosi wiki hii, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kama dhidi ya watani wa jadi, Simba SC, kwa sababu anatumikia adhabu.
Anaikosa mechi ya Mei 5, 2012- yaani Jumamosi wiki hii, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kama dhidi ya watani wa jadi, Simba SC, kwa sababu anatumikia adhabu.
Tegete atajiokoa mwenyewe kwa kuonyesha juhudi japo ligi imekwisha, timu itakapoanza maandalizi ya msimu mpya afanye vitu.
Lakini atajimaliza iwapo ataendele kuboronga na kuzidi kuwakatisha tamaa, wapenzi na wadau kwamba yeye basi tena.
Lakini atajimaliza iwapo ataendele kuboronga na kuzidi kuwakatisha tamaa, wapenzi na wadau kwamba yeye basi tena.
Tegete ana uzoefu mkubwa, achilia mbali wa mechi za kimataifa, pia wa mechi za watani wa jadi, hadi sasa
akiwa amefunga mabao matano katika mechi za watani, tangu ajiunge na timu hiyo
msimu wa 2008/2009 akitokea sekondari ya Makongo na timu ya taifa ya vijana
chini ya umri wa miaka 20.
‘Bismillah’ Tegete anatikisa nyavu za Simba ilikuwa Aprili 19, mwaka 2009
katika mechi ya marudiano ya Ligi Kuu ya Bara, iliyoisha kwa sare ya 2-2 Uwanja
wa Taifa, Dar es Salaam.
![]() |
| Tegete akielekezwa jambo na kocha Papic kabla ya kuingia kuifunga Simba kwa mara ya mwisho Oktoba 16, mwaka 2010 |
Tegete alifunga bao ambalo liliinusuru Yanga kuzama kwenye
mchezo huo kwa 2-1.
Lilikuwa bao zuri na la utata dakika ya mwisho kabisa,
akiunganisha krosi ya Mkenya Michael Barasa kutoka wingi ya kulia, ilionekana
kama ameunganisha mpira nyavuni kwa kichwa, lakini kumbe alipiga mpira kwa
ngumi, kwa ujanja wa hali ya juu na si refa wala mashabiki waliobaini hadi
marudio ya Televisheni baadaye.
Awali kwenye mchezo huo, kiungo Ramadhan Suleiman Chombo
‘Redondo’ alitangulia kuifungia Simba dakika ya 23, kabla ya Mkenya, Ben Mwalala
kusawazisha dakika ya 48 na
Haruna Moshi Shaaban ‘Boban’ kufunga la pili dakika ya 62.
Tegete akatikisa nyavu za Simba kwa mara ya pili Desemba 25, mwaka 2009
katika Nusu Fainali ya Kombe la Tusker, Yanga ikishinda 2-1 kwenye michuano ambayo
pamoja na kuipa timu yake Kombe, ikiifunga Sofapaka ya Kenya 2-1 kwenye
fainali, pia aliibuka mfungaji bpora.
Siku hiyo, Tegete aliwatungua Simba dakika ya 67 tu, lakini kiungo Mkenya, Hillary
‘Ford’ Echesa akawasawazishia Wekundu wa Msimbazi dakika ya 78 kwa penalti. Dakika 90 za mchezo ziliisha
kwa sare ya 1-1 na mechi ikahamia kwenye dakika 30 za nyongeza- na huko kiungo Shamte Ally Kilalile akaifungia
Yanga bao la ushindi, dakika ya mwisho kabisa Uwanja wa Taifa.
Tegete akawatungua tena mara mbili Aprili 18, mwaka 2010
katika mchezo wa marudiano wa Ligi Kuu, Yanga ikilala 4-3, dakika ya 69 na 89. Mabao
ya Simba yalifungwa na Uhuru
Suleiman Mwambungu dakika ya tatu, Mussa Hassan Mgosi dakika ya 53 na 74
na Hillary Echesa dakika ya 90 na ushei, wakati bao lingine la Yanga, lilifungwa na kiungo Athumani Iddi Athumani ‘Chuji’dakika ya 30.
Tegete aliifunga Simba kwa mara ya mwisho Oktoba 16, mwaka
2010, Uwanja wa CCM Kirumba mjini Mwanza, dakika ya 70, Yanga ikishinda 1-0. Siku
hiyo, Yanga ilicheza soka mbovu, lakini nafasi pekee nzuri aliyoipata kwenye
mechi iliyochezwa katika viunga alivyokulia vya Kirumba mjini Mwanza, Tegete
aliitumia vizuri kwa kukwamisha mpira nyavuni.
![]() |
| Tegete wa sasa aliyefulia, je msimu ujao ataibuka? |
Sasa ni miezi 19, yaani wastani wa miaka miwili imepita
Tegete hazijui nyavu za Simba na Jumamosi hachezi.
kwake hili ni pigo, lakini hapaswi kukata zaidi ya kuongeza juhudi ili msimu ujao arudi na cheche zake zile zilizomjengea heshima katika soka ya Tanzania.
kwake hili ni pigo, lakini hapaswi kukata zaidi ya kuongeza juhudi ili msimu ujao arudi na cheche zake zile zilizomjengea heshima katika soka ya Tanzania.
Tegete bado ni kijana mdogo maana yake bado ana nafasi ya kujiimarisha upya kisoka na kuwa tishio tena. Kikubwa ni juhudi, nidhamu na kujituma na kama kuna mahali anajua alikosea, akubali yeye ni binadamu na asikubali kurudia makosa.




.png)
0 comments:
Post a Comment