• HABARI MPYA

    Friday, May 04, 2012

    MIJI YA FAINALI ZA MATAIFA TA AFRIKA YATAJWA


    Host Cities for Orange CAN 2013 announced
    AFRIKA Kusini leo imetaja miji mtano itakayokuwa wenyeji wa Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika mwakani, inayotarajiwa kuanza Januari 19 hadi Februari 10, 2013.
    Majiji hayo matano ni Johannesburg katika Uwanja wa Soccer City, Port Elizabeth katika Uwanja wa Nelson Mandela Bay, Rustenburg katika Uwanja wa Royal Bafokeng, eThekwini katika Uwanja wa Moses Mabhida na Mbombela katika Uwanja wa Mbombela.
    Waziri wa Michezo wa Afrika Kusini, Fikile Mbalula pia alisema sherehe za ufunguzi na kufunga michuano hiyo, zitafanyika kwenye Uwanja wa Soccer City, Johannesburg.
    Pia, ratiba ya michuano hiyo itapangwa Oktoba 26, mwaka huu.
    Afrika Kusini walikuwa wenyeji wa Fainali za Mataifa ya Afrika mara moja tu mwaka 1996, walipoibuka mabingwwa na mwaka juzi, waliweka rekodi ya kuwa nchi ya kwanza ya Afrika kuwa mwenyeji wa Fainali za Kombe la Dunia
     .
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MIJI YA FAINALI ZA MATAIFA TA AFRIKA YATAJWA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top