• HABARI MPYA

    Saturday, May 19, 2012

    PREVIEW BAYEN MUNICH V CHELSEA LEO

    Mario Gomez wa Bayern
    Torres wa Chelsea
    Bayern wakipasha



    VIKOSI VYA LEO

    BAYERN MUNICH

    Neuer
    Lahm, Tymoshchuk, Boateng, Contento
    Schweinsteiger, Kroos
    Robben, Muller, RiberyGomez
    CHELSEA

    Cech
    Bosingwa, Cahill, David Luiz, Cole 
    Mikel, Essien
    Kalou, Lampard, MataDrogba

    WENYEJI Bayern Munich watawakosa wachezaji wake watatu wanaotumikia adhabu ya kadi, Holger Badstuber, David Alaba na Luiz Gustavo katika fainali la leo la Ligi ya Mabingwa dhidi ya Chelsea kwenye Uwanja wa Allianz Arena mjini Munich.

    Beki Breno anasumbuliwa na maumivu ya goti na atakuwa nje, Daniel Van Buyten hayuko fiti kwa mechi, hivyo Anatoliy Tymoshchuk na Diego Contento watabeba majukumu ya Badstuber na Alaba.

    Thomas Muller anaweza kurejea kwenye kikosi cha kwanza, na Toni Kroos atashuka kwenye kiungo cha ndani sambamba na Bastian Schweinsteiger.

    Chelsea watakuwa nao tena mabeki David Luiz na Gary Cahill, baada ya wawili kupona maumivu ya nyama za paja.

    Habari hizo ni njema kwa kocha wa Muda, Roberto Di Matteo, wakati ambao mabeki wake wa kawaida John Terry na Branislav Ivanovic wanatumikia adhabu ya kazi sambamba na Ramires na Raul Meireles.

    Winga Florent Malouda anayesumbuliwa na maumivu ya nyama za paja yuko shakani kucheza, wakati Didier Drogba anaweza kuanza na Fernando Torres mbele ya mdomo wa goli la wapinzani.

    JE WAJUA?

    • Bayern Munich imeshinda mechi zake 13 zilizopita kati ya 14 kwenye Uwanja wa Allianz Arena kwenye mashindano yote, nyingine wakitoa sare.
    • Kama The Bavarians watatwaa Kombe leo, wataungana na Liverpool kutwaa taji hilo mara tano, na kuingia kwenye orodha ya klabu zilizo nafasi ya tatu kwa mafanikio kwenye michuano hiyo, nyuma ya Real Madrid waliotwaa mara tisa na AC Milan mara saba.
    • Klabu hiyo ya Bundesliga ni ya kwanza kunufaika na Uwanja wa nyumbani kwenye fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, tangu Roma wacheze na Liverpool kwenye Uwanja wao wa Olimpico mwaka 1984.
    • Ushindi kwa Bayern utamfanya Jupp Heynckes (pichani kulia) kuwa kocha wa nne kushineda taji hilo na klabu mbili tofauti baada ya Ernst Happel, Ottmar Hitzfeld na Jose Mourinho.
    • Chelsea imeshinda mechi moja tu ya ugenini katika michuano hiyo msimu huu na tayari imefungwa na timu ya Ujerumani mabao 2-1, rejea kipigo cha Bayer Leverkusen katika hatua ya makundi.
    • Mechi ya mwisho kuikutanisha The Blues na Bayern ilikuwa katika Robo Fainali ya michuano hiyo mwaka 2005, na watoto wa London wakashinda kwa matokeo ya jumla 6-5.
    • Timu hiyo ya Ligi Kuu rekodi yake ya jumla dhidi ya timu za Ujerumani ni kushinda mechi 1, sare moja na kufungwa 4, huku ushindi wao pekee wakiupata dhidi ya Stuttgart msimu wa 2003-04 katika Ligi ya Mabingwa hatua ya 16 Bora.
    • Fainali pekee ya  michuano ya Ulaya kwa Chelsea ilikuwa mwaka 2008 mjini Moscow, ambako walifungwa  na Manchester United kwa penalti baada ya sare ya 1-1.
    Je, mambo yatakuwaje leo Allianz Arena? Bila shaka hilo ni jambo la kusubiri na kuona na BIN ZUBEIRY kama kawaida imetega mitambo yake sawasawaq kwenye Uwanja huo, tayari kuwahabarisha wasomaji wake A-Z ya game hilo.
    Chelsea wakipasha

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: PREVIEW BAYEN MUNICH V CHELSEA LEO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top