TIMU ya Ureno imeibuka na ushindi wa mabao 5–0 dhidi ya Uzbekistan katika mchezo wa Kundi K Fainali za Kombe la Dunia usiku huu Uwanja wa NRG, Houston, Texas nchini Marekani.
Mshambuliaji wa Al-Nassr ya Saudi Arabia, Cristiano Ronaldo dos Santos Aveiro alifunga mabao mawili dakika ya sita na 39 na kuweka rekodi ya kuwa mchezaji wa kwanza kufunga mabao kwenye Fainali sita mfululizo za Kombe la Dunia.
Beki wa kushoto wa Paris Saint-Germain, Nuno Alexandre Tavares mwenye asili ya Cape Verde akafunga bao la pili dakika ya 17, kabla ya kipa wa Nasaf ya Uzbekistan, Abduvohid Nematov kujifunga dakika ya 60 na winga wa AC Milan ya Italia, Rafael "Rafa" Alexandre da Conceição Leão mwenye asili ya Angola kufunga la tano dakika ya 87.
Mechi nyingine ya Kundi K itafuatia Saa 11:00 Alfajiri kati ya Colombia na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) Uwanja wa Akron Jijini Zapopan nchini Mexico.
Kwa sasa Ureno wapo kileleni kwa pointi zao nne za mechi mbili wakifuatiwa na Colombia yenye pointi tatu mechi moja na DRC pointi moja mechi moja – wakati Uzbekistan ambayo haina pointi inashika mkia.



.png)
0 comments:
Post a Comment