• HABARI MPYA

  Wednesday, June 14, 2017

  YANGA YAMSAJILI ‘NINJA’ WA ZENJI, NI MKOBA WA TAIFA JANG’OMBE

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  YANGA imemtambulisha mchezaji wa kwanza kabisa kumsajili kuelekea msimu ujao, ambaye ni beki Abdallah Hajji Shaibu ‘Ninja’ kutoka Taifa Jang’ombe ya Zanzibar.
  Katibu Mkuu wa Yanga, Charles Boniphace Mkwasa amesema beki huyo aliyeng’ara na kikosi cha Taifa Jang’ombe kwenye michuano ya Kombe la Mapinduzi Januari mwaka huu amesaini mkataba wa miaka miwili.
  Mkwasa amesema klabu imejiridhidha juu ya ubora wa beki huyo baada ya kupewa taarifa za awali za mchezaji huyo katika soka ya Zanzibar.
  Meneja wa Yanga, Hafidh Saleh (kulia) akimkabidhi jezi Abdallah Hajji Shaibu baada ya kusaini mkataba
  Katibu wa Yanga, Charles Boniphace Mkwasa akimshuhudia Abdallah Hajji Shaibu wakati anasaini
  Mkwasa amesema Yanga inaendelea na zoezi la usajili kwa umakini wa hali ya juu, ili kuhakikisha hairudii makosa ya kusajili wachezaji wasio na bidii wanageuka kuwa mzigo baadaye.
  Kwa ujumla Mkwasa amesema kwamba wanasajili kulingana na mapendekezo ya benchi la Ufundi, chini ya kocha wao mkuu, Mzambia George Lwandamina. 
  Kihistoria Zanzibar imekuwa na rekodi ya kutoa mabeki bora ambao wanakuja kuwika kwenye timu za Bara, mfano Kassim Issa aliyewika Mtibwa Sugar miaka ya 2000, Aggrey Morris anayeng’ara Azam FC, Nadir Haroub ‘Cannavaro’ ambaye ni Nahodha wa sasa wa Yanga anayecheza na Mzanzibari mwingine katika timu hiyo, Mwinyi Hajji Mngwali.
  Loading...
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: YANGA YAMSAJILI ‘NINJA’ WA ZENJI, NI MKOBA WA TAIFA JANG’OMBE Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top