• HABARI MPYA

  Tuesday, June 13, 2017

  WAKALI WA KOMEDI AFRIKA MASHARIKI KUPAGAWISHA TAMASHA LA EID EL FITRI

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  KAMPUNI ya Azam TV ya Dar es Salaam, imeandaa tamasha maalum la Eid El Fitri, litakalojulikana kama Eid Comedy Gala ambalo litafanyika siku ya Eid Mosi katika ukumbi wa King Solomon, uliopo Namanga, Dar es Salaam.
  Mratibu wa tamasha hilo, Yahya Mohammed amesema kwamba tamasha hilo litapambwa na burudani ya wachekeshaji maarufu Afrika Mashariki sambamba na muziki.
  Yahya amesema upande wa wachekeshaji watakuwapo wakali Eric Omondi kutoka Kenya, Herbert Ssegujja ‘Teacher Mpamire’ kutoka Uganda na wenyeji, Maulid Ali Fundi ‘Mau’ na Abdul Yussuf Machemba ‘Dogo Pepe’.
  Maulid Ali Fundi ‘Mau’ ni kati ya wasanii watakaotumbuiza tamasha la Eid Mosi 
  Mratibu wa tamasha, Yaya Mohammeed (kulia) akibadilishana mkataba na Abdul Yussuf Machemba ‘Dogo Pepe’
  Yahya amesema burudani ya muziki itaporomoshwa na bendi kongwe ya muziki wa vionjo ya Pwani, Njenje Band chini ya udhamini wa maji bora nchini, Uhai.
  “Matayarisho ya tamasha hili yanaendelea vizuri na lengo ni kuwakutanisha pamoja wapenzi wa Azam TV wa Dar es Salaam kusherehekea pamoja Eid El Fitri japo kwa uchache,”amesema.
  Kuhusu viingilio, Yahya amesema vitatajwa baadaye na amewataka watu kufuatilia chaneli za Azam TV kwa matangazo zaidi kuelekea tamasha hilo. “Waendelee kutazama chaneli zetu za Azam One, Two, Sinema Zetu, Azam Sports HD na nyingine ili kujua zaidi,”amesema.   
  Kwa upande wake, msanii nyota wa uchekeshaji nchini, Mau amefurahia kupata nafasi ya kuonyesha sanaa yake kwenye tamasha hilo na amewashukuru Azam TV. “Nawashukuru Azam TV kwa kunipa nafasi hii, na ninaahidi kufanya vizuri. Kikubwa tu ninawaomba watu wajitokeze kwa wingi siku hiyo,”amesema.   
  Loading...
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: WAKALI WA KOMEDI AFRIKA MASHARIKI KUPAGAWISHA TAMASHA LA EID EL FITRI Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top