• HABARI MPYA

    Monday, June 05, 2017

    WACHEZAJI ENGLAND 'WAFULIWA' JESHINI KUJIANDAA NA MECHI NA SCOTLAND

    KOCHA Gareth Southgate Ijumaa aliwapeleka wachezaji wa timu ya taifa ya England katika kambi ya Jeshi la wana maji kwa maandalizi ya mchezo ujao wa kufuzu Kombe la Dunia dhidi ya Scotland.
    Kocha huyo wa England aliwaondoa wachezaji wake St George's Park baada ya kuripoti kambini Ijumaa.
    Wachezaji wa England walipokonywa simu zao ili kuelekeza akili zao kwenye mazoezi hayo.
    Vijana wa Southgate walipewa mapumziko Jumatatu kabla ya kurejea St George's Park Jumanne. England itamenyana na Scotland mjini Glasgow Jumamosi, kabla ya kusafiri kwenda Ufaransa kwa mchezo wa kirafiki Jumanne ijayo.
    "Tulitaka kuja na kuwaweka vijana katika mazingira tofauti, kitu ambacho hawakukitarajia," alisema Southgate. 
    Winga wa England na Manchester City, Raheem Sterling akipewa mazoezi kwenye maji na wanajeshi Ijumaa PICHA ZAIDI GONGA HAPA 
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: WACHEZAJI ENGLAND 'WAFULIWA' JESHINI KUJIANDAA NA MECHI NA SCOTLAND Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top