• HABARI MPYA

    Wednesday, June 14, 2017

    UTARATIBU MPYA WA KUWAPATA MAWAKALA WA WACHEZAJI

    Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
    BAADA ya kufutwa utaratibu wa mawakala ‘agents’ wa wachezaji wa kulipwa, Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA), lilitangaza utaratibu mpya wa kukasimu majukumu hayo kwenye ngazi ya mashirikisho kwa kila taifa.
    Hivyo kwa mwaka 2016/2017, hakuna usajili wala uhamisho uliofanywa na watu wa kati yaani intermediaries wanaotambulika na TFF.
    TFF - Shirikisho la Soka Tanzania, linakwenda sambamba na utaratibu huo wa mabadiliko na kwa sasa linakamilisha mipango ya kusajili watu wa kati wa usajili watakaofahamika kama intermediaries.
    Usahili wa kati utatangazwa baada ya kikao cha Kamati ya Utendaji kitakachojadili kanuni za watu wa kati hapo baadaye.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: UTARATIBU MPYA WA KUWAPATA MAWAKALA WA WACHEZAJI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top