• HABARI MPYA

    Tuesday, June 06, 2017

    TURAN AFUKUZWA TIMU YA TAIFA KWA KUMTWANGA MWANDISHI

    KIUNGO wa Barcelona, Arda Turan amestaafu soka ya kimataifa baada ya kuenguliwa kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Uturuki kwa kosa la kumpiga mwandishi wa habari kwenye ndege.
    "Nafikiri wakati umefika...nahitimisha kuichezea timu ya taifa,"amesema mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 30, kiungo wa Barcelona, ambaye ameichezea Uturuki mechi 96 katika mkutano wake mfupi na Waandishi wa Habari Slovenia uliorushwa na Televisheni Uturuki television.
    Gazeti la kila siku la Hürriyet la Uturuki limeripoti leo kwamba Turan alimpiga kichwa mwandishi wa habari wakirejea kutoka Skopje, ambako Uturuki ilitoka sare ya 0-0 na Macedonia.

    Kiungo wa Barcelona, Arda Turan ameamua kustaafu soka ya kimataifa baada ya kuenguliwa kikosi cha Uturuki kwa kumpoga mwandishi wa habari kwenye ndege PICHA ZAIDI GONGA HAPA  

    Walikuwa wanataka kupaa kwenda Italia ambako wataweka kambi ya mazoezi kujiandaa na mchezo dhidi ya Kosovo Jumapili wakati Turan alipomfuata mwandishi huyo wa habari kwenye ndege, ambaye aliandika habari kuhusu kiungo huyo mwenye umri wa miaka 30 wakati wa michuano ya Euro 2016. 
    Kabla ndege haijaruka, aliripotiwa kumuita mwandishi mkongwe wa habari, Bilal Mese kumuuliza kuhusu habari aliyoandika kuhusu wachezaji wa Uturuki mwaka jana kwamba walitaka posho kubwa ili kuichezea nchi yao kwenye mashindano.
    Hürriyet liliripoti Turan aliseema: "Niambie Bilal Mese, wewe ulikuwepo pale? Ulikuwa na sisi wakati unaandika habari za posho? Nani nilimuomba fedha kutoka wapi? Nani nilimuomba posho kutoka wapi? Ongea. Njoo. Nani amekufanya uandike hizo taarifa?"
    Hürriyet limedai kwamba Turan aliendelea kumpa kibano mwandishi huyo bila hatua yoyote kuchukuliwa na kiongozi wa timu, Fatih Terim, ambaye pia alikuwepo kwenye ndege. Kiungo huyo wa Barcelona ameripotiwa kusema; "Ni aina gani ya nchi hii? Wamekuruhusu kwenye ndege hii. K*** hao waliokuruhusu kupanda hii ndege.
    "Unafikiri nilikuwa kama wengine. Nani nilimuomba fedha kutoka wapi? Wewe mwanaharamu. Bora nistaafu soka kuliko kumruhusu yeyote kusema chochote dhidi ya heshima yangu, famililia yangu,"alisema.
    Turan alimbwatukia hadi Rais wa Shirikisho la Soka Uturuki, Yildirim Demiroren na kudai kwamba yeye ndiye aliyesababisha habari zile kuandikwa kwa sababu anamiliki gazeti lile lililowaandika wao.
    Taarifa nyingine zinasema kwamba Turan alimvaa mwandishi huyo na kuanza kumpiga kabla ya kudhibitiwa na wachezaji wenzake.
    Lakini hakuonyesha kusikitikia hilo katika taarifa yake aliposti kwenye ukurasa wake wa Instagram: "Nilifanya sahihi jana? Sijui!!! Labda si sahihi, lakini angalau uwazi, heshima, adabu kubwa... Nilipata jibu? Hapana.. [Yeye] amejaza kurasa kwa mwezi mzima, lakini mbele yangu hakuwa na zaidi ya maneno mawili.'
    Baada ta kukutana na Ofisa mkubwa wa Shirikisho la Soka Uturuki, imeripotiwa Turan alitakiwa kuondoka kwenye hoteli ya timu na hatashirikishwa kwenye mchezo wa Jumapili.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: TURAN AFUKUZWA TIMU YA TAIFA KWA KUMTWANGA MWANDISHI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top