• HABARI MPYA

  Monday, June 05, 2017

  SINGIDA UNITED YATOLEWA MAPEMA SPORTPESA SUPER CUP

  Na Rehema Lucas, DAR ES SALAAM 
  TIMU ya AFC Leopard ‘Ingwe’ imekuwa ya kwanza kwenda Nusu Fainali ya SportPesa Super Cup baada ya ushindi wa penalti 5-4 kufuatia sare ya 1-1 ndani ya dakika 90.
  Beki Salum Chukwu aliyesajiliwa kutoka Toto Africans alifanya kazi nzuri ya kuwadhibiti washambuliaji wa Ingwe, lakini akaenda kupiga juu ya lango mkwaju wake wa penalti.
  Waliotumbukiza kambani matuta ya AFC Leopard ni Bernard Mangoli, Marselas Ingotsi, Kateregga Allan, Duncan Otieno na Fiamenyo Gilbert, wakati za Singida zilifungwa na Atupele Green, Hamisi Shengo, Nhivi Simbarashe na Muroiwa Elisha.
  Kocha wa Singida United, Mholanzi Hans van der Pluijm akifuatilia mchezo leo 
  Hamisi Shengo wa Singida United (kulia) akijaribu kumpita beki wa AFC Leopards, Michael Kibwage 

  Singida United inayofundishwa na kocha Mholanzi, Hans van der Pluijm ilikuwa ya kwanza kupata bao dakika ya 20 kupitia kwa Mzimbabwe Kutinyu Tafadzwa, kabla ya Ingwe kusawazisha kupitia kwa Vincent Oburu dakika ya 63.
  Baada ya hapo, timu zote ziliendelea kushambuliana kwa zamu na kosa kosa za pande zote mbili hadi mchezio kuamuliwa kwa mikwaju ya penalti.
  Kwa matokeo hayo, AFC Leopard atakutana na mshindi kati ya Yanga na Tusker ya Kenya pia zinazomenyana muda huu katika mchezo wa michuano hiyo.
  Kikosi cha Singida United kilikuwa; Lubawa Said, Muroiwa Elisha, Msonjo Roland, Dumba Hassan, Chukwu Salum, Ally Kenny, Mtasa Wisdom, Kutinyu Tafadzwa/ Kagoma Yussuf dk85, Green Atupele, Nhivi Simbarashe/ Nizar Khalfan dk 75 na Shengo Hamisi.
  AFC Leopards; Gabriel Andika, Dennis Sikhai, Marcus Abwao, Abdallah Salim, Duncan Otieno, Isuza Whyvonne, Mangoli Bernard, Joshua Mawira, Fiamenyo Gilbert, Haron Nyakha/Allan Kateregga dk63 na Vincent Oburu.
  Loading...
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SINGIDA UNITED YATOLEWA MAPEMA SPORTPESA SUPER CUP Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top