• HABARI MPYA

  Friday, June 09, 2017

  SAMATTA: AFE KIPA, AFE BEKI LESOTHO LAZIMA WAKAE CHAMAZI KESHO

  Na Rehema Lucas, DAR ES SALAAM
  NAHODHA wa Tanzania, Mbwana Ally Samatta amesema kwamba kwa vyovyote vile kesho lazima washinde dhidi ya Lesotho.
  Taifa Stars watawakaribisha Mamba kesho kuanzia Saa 2:00 usiku Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam katika mchezo wa kwanza wa Kundi L kufuzu Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika mwaka 2019.
  Na Samatta anayechezea KRC Genk ya Ubelgiji amesema; “Afe kipa, afe beki lazima tuifunge Lesotho kesho,”.
  Jeuri ya Samatta kuwatangazia ubabe mapema Lesotho inatokana na maandalizi ya timu kwa ajili ya mchezo huo na zaidi anashukuru yeye kama Nahodha wa timu yuko vizuri kuelekea mchezo huo.

  Mbwana Samatta (kushoto) amesema kwamba kwa vyovyote vile kesho lazima washinde dhidi ya Lesotho

  “Nimejiandaa vizuri kwa mechi ya kesho dhidi ya Lesotho na wachezaji wenzangu wote wapo vizuri na nina uhakika kambi walioiweka nchini Misri wamefanya mazoezi ya kutosha na tutafanya vizuri japo mechezo huu hautakuwa mwepesi,”amesema.
  Kwa upande wake, kocha mkuu wa Taifa Stars, Salum Mayanga amesema kwamba timu imemaliza salama mazoezi na wana imani kesho watafanya vizuri.
  “Timu imemaliza salama mazoezi leo asubuhi, hali za vijana ni nzuri na nina imani tutafanya vizuri na tutapata ushindi na tunaiheshimu Lesotho, kwa sababu ukiangalia mechi za nyuma zote wamefanya vizuri hivyo tutajitahidi kufanya vizuri kwenye mchezo wa kesho,”amesema Mayanga.
  Taifa Stars itaingia kwenye mchezo wa kesho ikitoka kwenye kambi ya wiki moja nchini Misri na kwa ujumla huio utakuwa mchezo wa tatu kwa Mayanga tangu arithi mikoba ya Charles Boniface Mkwasa baada ya Machi mwaka huu kushinda 2-0 dhidi ya Botswana na 2-1 dhidi ya Burundi.
  Loading...
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SAMATTA: AFE KIPA, AFE BEKI LESOTHO LAZIMA WAKAE CHAMAZI KESHO Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top