• HABARI MPYA

  Sunday, June 04, 2017

  NGASSA KUICHEZEA YANGA SPORTPESA SUPER CUP

  Na Princess Asia, DAR ES SALAAM
  KIUNGO Mrisho Khalfan Ngassa amerudi nyumbani, Yanga SC na kesho anatarajiwa kuichezea timu hiyo katika mchezo wa kwanza wa michuano ya SportPesa Super Cup dhidi ya Tusker FC ya Kenya kuanzia Saa 10:00 jioni Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.  
  Michuano ya SportPesa Super Cup inatarajiwa kuanza kesho Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam na Ngassa wa Mbeya City FC ni kati ya wachezaji waalikwa watakaopewa nafasi kwenye kikosi cha Yanga.
  Mrisho Ngassa ataichezea Yanga katika mchezo wa kwanza wa michuano ya SportPesa Super Cup dhidi ya Tusker FC ya Kenya kesho

  Japokuwa inaelezwa hiyo ndiyo moja kwa moja safari ya kurejea nyumbani, Jangwani baada ya miaka miwili, lakini Ngassa ataichezea Yanga kwa ruhusa ya uongozi wa timu yake ya sasa, Mbeya City. 
  Ngassa aliondoka Yanga Mei mwaka 2015 kuhamia Free State Stars ya Afrika Kusini ambako alicheza hadi Agosti mwaka jana alipokwenda kujiunga na Fanja ya Oman, ambako alidumu kwa mwezi mmoja tu na kurejea nyumbani kujiunga na Mbeya City kwa mkataba wa mwaka mmoja.
  Na baada ya kuichezea kwa nusu msimu Mbeya City, tayari kuna dalili za Ngassa kurejea tena Yanga, timu ambayo wazi anaipenda kwa dhati.
  Ni kiwango chake katika michuano hii ya SportPesa Super Cup ndicho kitaamua hatima yake katika mpangon wake kurejea Yanga. 
  Ngassa alijiunga na Yanga SC kwa mara ya kwanza mwaka 2007 na akacheza hadi mwaka 2010 alipohamia Azam FC, kabla ya kurejea mwaka 2013 na kucheza hadi 2015 alipoondoka tena.
  Loading...
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: NGASSA KUICHEZEA YANGA SPORTPESA SUPER CUP Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top