• HABARI MPYA

  Thursday, June 08, 2017

  MAGWIJI MAN UTD KUWAVAA BARCA SEPT 2 OLD TRAFFORD

  MAGWIJI wa Manchester United watarejea Uwanja wa Old Trafford Jumamosi ya Septemba 2, mwaka 2017 kwa mechi dhidi ya magwiji wa Barcelona itakayoanza Saa 9:00 Alasiri.
  Tovuti rasmi ya Man United imeandika kwamba katika mchezo huo, Andrew 'Andy' Cole atarejea kama Kocha Msaidizi wa Bryan Robson na anatarajiwa kujichanganya na waxchezaji.
  "Sitakuwa nawafokea tu wachezaji kwenye benchi, lakini nitakuwa nawahamasisha na kucheka nao. Itakuwa siku nzuri," alisema Cole.
  Kikosi hicho kinawahusisha Quinton Fortune, Edwin van der Sar, Paul Scholes, Denis Irwin, Dwight Yorke, Phil Neville, Ronny Johnsen, Louis Saha, Mikaël Silvestre, Jesper Blomqvist na Dion Dublin.
  Upande wa timu ya Katalunya itakayoongozwa na kocha Jose Mari Bakero, kitakuwa na wakali wa zamani kama Gaizka Mendieta, Eric Abidal, Miguel Angel Nadal, Gheorghe Popescu, Andoni Goikoetxea na Julio Salinas.
  Tukio hilo litahusisha burudani ya muziki pia kutoka vikundi na wasanii mbalimbali pamoja na sherehe za kifamilia nje ya Uwanja.
  Loading...
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MAGWIJI MAN UTD KUWAVAA BARCA SEPT 2 OLD TRAFFORD Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top