• HABARI MPYA

  Tuesday, June 13, 2017

  IRAN YA PILI KUFUZU KOMBE LA DUNIA BAADA YA BRAZIL

  TEHRAN, Iran 
  TIMU ya taifa ya Iran imekuwa ya pili kufuzu Fainali za Kombe la Dunia mwakani nchini Urusi baada ya kuifunga Uzbekistan 2-0 usiku wa jana na kuwapa furaha mashabiki wake kumwagika mitaani kushangilia.
  Hii ni mara ya kwanza Iran inafuzu mfululizo kwenye fainali za Kombe la Dunia na kwa ujumla watashiriki fainali za michuano hiyo kwa mara ya tano.
  Sardar Azmoun alifunga bao la kwanza dakika ya 23 na Mehdi Taremi akafunga la pili dakika ya 88 Uwanja wa Azadi mjini Tehran.
  Wachezaji wa Iran wakifurahia kufuzu Fainali za Kombe la Dunia mwakani nchini Urusi baada ya kuifunga Uzbekistan 2-0 usiku wa jana

  Iran inayofundishwa na kocha wa zamani wa Real Madrid na Ureno, Carlos Queiroz tangu mwaka 2011, imeongoza Kundi A kwa Asian kufuzu Kombe la Dunia. 
  Timu hiyo imecheza mechi nane bila kupoteza hata moja na inaizidi kwa pointi nane, Uzbekistan iliyo katika nafasi ya tatu nyuma ya Korea Kusini iliyo nafasi ya pili.
  Iran haijaruhusu nyavu zake kuguswa kwenye mechi za kufuzu hadi sasa, jambo ambalo linawajengea hali ya kujiamini mashabiki wake.
  Loading...
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: IRAN YA PILI KUFUZU KOMBE LA DUNIA BAADA YA BRAZIL Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top