KOCHA mpya wa Manchester United hakuwepo kwenye mkutamo wa makocha babu kubwa duniani wa kila mwaka, uliofanyika mjini Nyon, Usiwsi.
Jana na leo, kocha wa zamani wa Manchester United, Sir Alex Ferguson amekuwa Mwenyekiti wa Mkutano wa 16 wa makocha duniani, ujulikanao kama Elite Club Coaches Forum kama balozi wa makocha wa UEFA ambao ulihudhuriwa pia na rais wa shirikisho hilo la soka Ulaya, Michel Platini.
Ferguson alipigwa picha akitaniana na mpinzani wake wa zamani kazini Arsene Wenger wa Arsenal, wakati kocha wa Manchester City, Manuel Pellegrini alikuwepo pia.
Picha ya timu:Mkutano wa Makocha uliofanyika makao makuu ya UEFA nchini Usiwsi (akiwemo Pep Guardiola na Luis Enrique)
Kocha wa Chelsea, Jose Mourinho amehudhuria mkutano huo pamoja na makocha wa zamani wa Stamford Bridge, Andre Villas-Boas, Rafael Bentiez na Carlo Ancelotti.
Luis Enrique aliketi jirani na kocha wa zamani wa Barcelona, Pep Guardiola katika picha ya pamoja.
Sir Alex Ferguson akizungumza na Carlo Ancelotti na Arsene Wenger katika mkutano huo mjini Nyon
Kocha wa Chelsea, Jose Mourinho na kocha wa zamani wa Stamford Bridge, Carlo Ancelotti



.png)
0 comments:
Post a Comment