• HABARI MPYA

    Saturday, September 13, 2014

    SHINJI KAGAWA AREJEA KWA KISHINDO BUNDESLIGA, APGA BAO NA KUSETI MOJA DORTMUND IKISHINDA 3-1

    KIUNGO Shinji Kagawa amerejea kwa kishindo Bundesliga baada ya mchezaji huyo wa zamani wa Manchester United kufunga bao na kutoa pasi katika ushindi wa 3-1 wa Borussia Dortmund dhidi ya Freburg leo akicheza mechi ya pili tangu arudi 'nyumbani'.
    Mwanasoka huyo wa kimataifa wa Japan alimsetia Adrian Ramos kufunga bao la kwanza dakika ya 34, kabla ya yeye mwenyewe la pili kana ya mapumziko.
    Kagawa alipata mapokezi mazuri akirejea Wesfalenstadion, ambako mashabiki walibeba mabango na bendera zenye picha yake na kumshangilia ile mbaya wakiimba jina lake.
    Huku ndio nyumbani; Shinji Kagawa akishangilia baada ya katika mechi ya Bundesliga

    Aliondoka Dortmund kuhamia United mwaka 2012, lakini akashindwa kung'ara na kuwashawishi makocha wa timu hiyo kumpa nafasi ya kudumu kwenye kikosi cha kwanza Old Traffford baada ya kusajiliwa kwa Pauni Milioni 12.
    Nyota huyo mwenye umri wa miaka 25 msimu ameuzwa na kocha Louis van Gaal kwa dau la hasara la Pauni Milioni 6.3 akiungana tena na kocha Jurgen Klopp, ambaye alisema alitamani kumwaga machozi namna mchezaji huyo alivyokuwa anagfanyiwa United.
    Dortmund tayari imeuaza jezi 5,000 za Kagawa baada ya kiungo huyo kurejea klabuni. Dortmund's Shinji Kagawa  and Freiburg's Julian Schuster challenge for the ball during
    Shinji Kagawa akitafita mbinu za kumtoka Julian Schuster 
    Shinji Kagawa of Dortmund is welcomed back by supporters prior to the Bundesliga match
    Shabiki akiwa amebeba bang la picha ya Shinji Kagawa leo
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: SHINJI KAGAWA AREJEA KWA KISHINDO BUNDESLIGA, APGA BAO NA KUSETI MOJA DORTMUND IKISHINDA 3-1 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top