• HABARI MPYA

    Friday, September 05, 2014

    PIGO CHELSEA; DIEGO COSTA AUMIA TENA NYAMA NA KUTEMWA KIKOSI CHA HISPANIA

    MSHAMBULIAJI wa Chelsea, Diego Costa ameondolewa kwenye kikosi cha Hispania kitakachocheza mechi ya kuwania kufuzu kwenye fainali za Euro dhidi ya Macedonia kutokana na maumivu ya nyama za paka.
    Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25 alisumbuliwa na matatizo kama hayo kwa miezi minne iliyopita na alilazimika kutolewa kwenye kikosi cha Hispania kilichofungwa 1-0 na Ufaransa katika mchezo wa kirafiki jana baada ya kuhisi maumivu.
    Munir El Haddadi, mchezaji mwenye thamani kubwa wa Barcelona, ataziba pengo la Costa katika mchezo huo utakaofanyika Jumatatu mjini Valencia.
    Majeruhi: Diego Costa ameondolewa kikosi cha Hispania baada ya kuumia nyama
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: PIGO CHELSEA; DIEGO COSTA AUMIA TENA NYAMA NA KUTEMWA KIKOSI CHA HISPANIA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top