• HABARI MPYA

    Saturday, September 06, 2014

    MANNY PACQUIAO ASEMA; "SASA PAMBANO LA MIMI NA MAYWEATHER LINAKUJA"

    BONDIA Manny Pacquiao amesema majadiliano yanaendelea juu ya bambino la Pauni Milioni 300 baina yake na Floyd Mayweather Jnr.
    Mabingwa hao wawili wa uzito wa Welter duniani, kwa muda mrefu wamekuwa wakichukuliwa kama mabondia bora zaidi duniani.
    Lakini mashabiki wa ngumi wamekuwa wakisikitishwa na kitendo cha wawili huo kutofikia makubaliano ya kukutana ulingoni kwa ajili ya pambano linallotarajiwa kuwa la utajiri mkubwa zaidi kihistoria.
    Pambano la wakali; Floyd Mayweather Jr anaweza kuzipiga na Manny Pacquiao mwakani 
    Ongoing: Pacquiao (right) says negotiations have begun over a fight with Mayweather in 2015
    Mjadala unaendelea: Pacquiao (kulia) amesema kuna majadiliano yameanza kwa ajili ya pambano na Mayweather mwaka 2015

      Akizungumza wakati wa Mkutano na Waandishi wa Habari kupromoti pambano lake na Chris Algieri mwezi Novemba, Pacquiao amesema: "Kuna majadiliano makini na kambi ya Mayweather na promota wangu,".
      Alipoulizwa iwapo pambano hilo litafanyika Mei, akasema: "Uwezekano kwa mwakani,".
      Promota wa Pacquiao, Bob Arum amesema hive karibuni kwamba anaamini mabondia hao watapigana mara mbili mwaka 2015.
      "Mitandao tote ya Televisheni intake pambano hili like  dalili zote zinalenga pambano la kwanza mapema mwakani, pambano la pili litakuja na dau tofauti, kwa sababu mshindi wa pambano la kwanza atadai fedha nyingi. Na kwa kuwa kila mmoja kati yao anaamini atashinda, hiyo inaleta mlolongo zaidi,".
      Mayweather, wakati huo huo ameelekeza fikra zake katika pambano lake la marudiano na Marcos Maidana mjini Las Vegas Jumamosi wiki ijayo.
      Amebakiza mapambano matatu katika Mkataba wake wa dola za Kimarekani Milioni 200 na Showtime, huku mengine yakitarajiwa kufanyika May na Septemba mwakani.
      Pacquiao amesema amepanga kustaafu mwaka 2016 na kuelekeza nguvu zake zaidi katika siasa za nchini mwake, Philippines. 
      • Blogger Comments
      • Facebook Comments

      0 comments:

      Item Reviewed: MANNY PACQUIAO ASEMA; "SASA PAMBANO LA MIMI NA MAYWEATHER LINAKUJA" Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
      Scroll to Top