BEKI wa pembeni wa Arsenal, Mfaransa Mathieu Debuchy anaweza kuwa nje ya Uwanja hadi Krisimasi baada ya kuumia enka dhidi ya Manchester City mwishoni mwa wiki iliyopita.
Kocha Arsene Wenger amesema kwamba Debuchy alitarajiwa kwenda kufanyiwa uchunguzi kama atahitaji upausaji wa kifundo chake cha mguu jana jioni ambao utatoa majibu atakaa nje kwa muda gani.
Ikiwa hatahitaji upasuaji, itamchukua wiki sita nje ya Uwanja kabla ya kurejea dimbani, lakini kama atapigwa 'kisu' atakuwa nje kwa angalau miezi mitatu.
0 comments:
Post a Comment