YANGA SC imesajili wachezaji wawili kutoka Brazil, kiungo Andery Coutinho na mshambuliaji Geilson Santana Santos ‘Jaja’ ambao hadi sasa kila mmoja amekwishacheza mechi nne na kufunga mabao mawili.
Kwa ambaye hajawaona wachezaji hao na anawasikia tu, akiambiwa wamefunga mabao mawili katika mechi nne, hatawatilia shaka juu ya uwezo wao.
Lakini kwa wapenzi wa Yanga SC wenyewe ambao wamewaona wachezaji wao, wamevutiwa mno na Coutinho, ila kwa Jaja hawajamkubali.
Na mitazamo ya wengi miongoni mwa wachambuzi na wataalamu wa soka, haipishani sana na wapenzi wa Yanga SC.
Japokuwa Jaja amefunga bao pekee mara mbili, Yanga SC ikishinda 1-0 dhidi ya Chipukizi Uwanja wa Gombani, Pemba na 1-0 tena dhidi ya Thika United Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, uchezaji wake haujavutia.
Ni mzito hawezi hata kurukia mipira ya juu, hawezi kujivuta kuifuata pasi ambayo iko mbali naye kidogo hata kwa hatua moja.
Na hata mipira anayofikishiwa kwenye himaya yake, michache anayoweza kuimiliki vyema na amekuwa mwepesi kutoa pasi kila anapofikishiwa mpira, jambo ambalo limejenga hisia anaogopa mipira, anaogopa kuharibu.
Yanga SC wanahisi wanaipoteza nafasi hiyo moja ya mchezaji wa kigeni kati ya tano tu, wakati wakitazama upande wa pili, wapinzani wao Simba na Azam wana wachezaji wazuri wa kigeni.
Kwa kuufikiria upinzani wa Ligi Kuu inayoanza ndani ya wiki mbili tangu sasa, kwa hakika wana Yanga wanaona kabisa wanajiweka katika mazingira magumu.
Hakuna wasiwasi kuhusu Coutinho, huyo wamemkubali kwa asilimia 100. Iliripotiwa viongozi wa Yanga SC walitaka mchezaji huyo akatwe ili asajiliwe mgeni mwingine, lakini kocha Mbrazil aliyewaleta wachezaji hao, Marcio Maximo akagoma.
Si kugoma tu, inadaiwa Maximo pia alitishia kuondoka iwapo mchezaji huyo atakatwa na ndipo viongozi walipokuwa wapole na sasa Jaja ni mchezaji kwenye ordha ya wachezaji Yanga SC.
Na Maximo ameonyesha imani kubwa kwa mchezaji huyo, akimuanzisha katika mechi zote na kumpa nafasi zaidi uwanjani.
Kana kwamba hiyo haitoshi, anawaambia Yanga SC wakitaka kuona chenga na ladha nyingine za kisoka wawatazame wachezaji wengine kama Haruna Niyonzima, lakini kushangilia mabao wasubiri kutoka kwa Jaja.
Maximo anakwenda mbali zaidi, akimfananisha Jaja na mshambuliaji wa kimataifa wa Ujerumani, Toni Kroos kwamba yeye anajua kufunga tu.
Maximo ni kocha mzoefu, ambaye awali amefanya kazi Tanzania kama kocha wa Taifa Stars kuanzia 2006 hadi 2010 na ndio wakati ambao alijizolea wapenzi wengi nchini.
Akiwa Taifa Stars, Maximo alimuita kikosini mchezaji Jerry Tegete akiwa mdogo sana na japokuwa alikuwa hachezi kiasi cha wananchi kuanza kulalamika, baadaye mshambuliaji huyo akawa tegemeo la mabao Stars kabla ya kushuka kiwango siku za karibuni.
Maximo alikuwa anamchukua Taifa Stars, mshambuliaji Gaudene Mwaikimba huku wananchi wakilalamika anabeba galasa, akiacha wakali kama Emmanuel Gabriel.
Baadaye kwa shinikizo, akamuita Gabriel lakini kwa bahati mbaya hakuwa na msaada kwenye timu.
Maximo alikuja Tanzania, kipa namba moja akiwa Juma Kaseja, lakini akaamua kuanza kumtumia Ivo Mapunda ambaye wananchi walikuwa hawamkubali sana.
Ni Maximo huyo huyo alikataa kumuita Taifa Stars Mrisho Ngassa badala yake akimuita Vincent Barnabas hadi baadaye sana alipoamua kumchukua na akawa tegemeo la taifa hadi leo.
Maximo ni kocha mwenye misimamo, falsafa na mitazamo ya aina yake ambayo ni vigumu kumuelewa mapema.
Ni kama sasa misimamo yake kwa Jaja, wengi hawamuelewi- lakini bora tu wana Yanga SC wampe muda, kwa sababu klabu hiyo imekwishasajili wachezaji wengi inayoamini ni wazuri, na haijafanya kipya katika ulimwengu wa soka zaidi ya ubingwa wa Bara na kutolewa mapema michuano ya Afrika. Alamsiki.

0 comments:
Post a Comment