Na Mahmoud Zubeiry, DAR ES SALAAM
KOCHA Marcio Maximo amemuanzisha mshambuliaji Genilson Santana ‘Jaja’ wakati Simon Msuva na Said Bahanuzi hawajahusishwa kabisa katika mchezo wa Ngao ya Jamii dhidi ya Azam FC unaotarajiwa kuanza Saa 10:30 Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Simon Msuva amevaa jezi na anafanya mazoezi ya awali kabla ya mchezo muda huu, lakini Bahanuzi amepanda jukwaani kabisa, ingawa yeye mwenyewe anasema yuko fiti.
Kiungo Andrey Coutinho ameshindwa kabisa kucheza naye yuko jukwaani, baada ya kuumia katikati ya wiki katika mchezo wa kirafiki dhidi ya Polisi Uwanja wa sekondari ya Loyola, Mabibo, Dar es Salaam.
Kikosi cha Yanga SC kinachoazna ni; Deo Munishi ‘Dida’, Juma Abdul, Oscar Joshua, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Kevin Yondan, Mbuyu Twite, Said ‘Kizota’ Juma, Haruna Niyonzima, Genilson Santana ‘Jaja’, Mrisho Ngassa na Nizar Khlafan.
Azam FC; Mwadini Ali, Erasto Nyoni, Shomary Kapombe, David Mwantika, Aggrey Morris, Kipre Balou, Himid Mao, Salum Abubakar ‘Sure Boy’, Didier Kavumbangu, Kipre Tchetche na Leonel Saint-Preux.

![]() |
Genilson Santana 'Jaja' anaanza leo kikosi cha kwanza Yanga |
![]() |
Simon Msuva kushoto hayumo kabisa kwenye mchezo wa leo |
Kikosi cha Yanga SC kinachoazna ni; Deo Munishi ‘Dida’, Juma Abdul, Oscar Joshua, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Kevin Yondan, Mbuyu Twite, Said ‘Kizota’ Juma, Haruna Niyonzima, Genilson Santana ‘Jaja’, Mrisho Ngassa na Nizar Khlafan.
Azam FC; Mwadini Ali, Erasto Nyoni, Shomary Kapombe, David Mwantika, Aggrey Morris, Kipre Balou, Himid Mao, Salum Abubakar ‘Sure Boy’, Didier Kavumbangu, Kipre Tchetche na Leonel Saint-Preux.
0 comments:
Post a Comment