• HABARI MPYA

    Saturday, September 13, 2014

    MAN CITY CHUPUCHUPU KWA ARSENAL, YACHOMOA DAKIKA ZA LALA SALAMA EMIRATES

    BAO la dakika ya 83 la Martin Demichelis limeinusuru Manchester City kulala mbele ya Arsenal baada ya kupata sare ya kufungana mabao 2-2 Uwanja wa Emirates katika mchezo wa Ligi Kuu ya England jioni ya leo.
    Sergio Aguero alitangulia kuifungia City dakika ya 28 akimalizia kazi nzuri ya Jesus Navas kabla ya Jack Wilshere kuisawazishia Arsenal kipindi cha pili akimalizia kazi nzuri ya Aaron Ramsey
    Lingekuwa la ushindi; Alexis Sanchez akishangilia baada ya kuifungia bao la pili Arsenal 

    Alexis Sanchez akaifungia Arsenal bao la pili dakika ya 74 kabla ya Debuchy kuisawaishia City. Mshambuliaji mpya wa Arsenal, Danny Welbeck alikaribia kufunga dakika ya 11 baada ya kugongesha mwamba, wakati kiungo mpya wa Man City, Frank Lampard alionyeshwa kadi ya njano.
    Kikosi cha Arsenal kilikuwa: Szczesny, Debuchy/Chambers dk81, Mertesacker, Koscielny, Monreal, Flamini/Arteta dk95, Wilshere, Ramsey, Alexis, Ozil na Welbeck/Oxlade-Chamberlain dk88.
    Man City: Hart, Zabaleta, Kompany, Demichelis, Clichy, Fernandinho/Kolarov dk77, Lampard/Nasri dk45, Navas, Silva, Milner, Aguero/Dzeko dk67.
    Sergio Aguero akishangilia baada ya kuifungia Manchester City
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MAN CITY CHUPUCHUPU KWA ARSENAL, YACHOMOA DAKIKA ZA LALA SALAMA EMIRATES Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top