• HABARI MPYA

    Friday, September 05, 2014

    MAJERUHI KOMPANY AGONGA ZOTE 90 UBELGIJI IKISHINDA 2-0

    BEKI Vincent Kompany jana amecheza kwa dakika zote 90, Ubelgiji ikishinda mabao 2-0 dhidi ya Australia katika mchezo wa kirafiki, licha ya wasiwasi kwamba alikuwa majeruhi.
    Beki huyo wa Manchester City alikuwa shakani kucheza mechi hiyo ya kirafiki ya kimataifa mjini Liege, baada ya kubaki kwenye mazoezi ya Jumatano.
    Ubelgiji ilipata ushindi huo kutokana na mabao ya Dries Mertens dakika ya 18 na Axel Witsel dakika ya 77.

    Mtu wa kazi; Vincent Kompany kulia amecheza kwa dakika zote 90 jana Ubelgiji ikishinda 2-0 dhidi ya Australia 
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MAJERUHI KOMPANY AGONGA ZOTE 90 UBELGIJI IKISHINDA 2-0 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top