• HABARI MPYA

    Friday, September 05, 2014

    LOIC REMY ASHEREHEKEA KUTUA CHELSEA KWA KUIPIGIA BAO LA USHINDI UFARANSA DHIDI YA HISPANIA

    MSHAMBULIAJI Loic Remy amesherehekea kuhamia kwake Chelsea kwa kufunga bao pekee la ushindi Ufaransa ikiilaza Hispania 1-0 katika mchezo wa kirafiki wa kimataifa.
    Mchezaji huyo wa zamani wa QPR alitokea benchi kwenda kufunga bao hilo pekee zikiwa zimesalia dakika 16 mchezo kumalizika, akimtungua vizuri kipa wa Manchester United, David de Gea kumpa raha kocha Didier Deschamps Uwanja wa Stade de France.
    Hispania ilitawala mchezo, lakini ikashindwa tu kutikisa nyavu za wenyeji huku kipa Hugo Lloris akiwas kikwazo kikuu kwao. 
    Remy Roketi: Mfungaji wa bao pekee la Ufaransa, Loic Remy akishangilia na Moussa Sissoko na Mathieu Valbuena
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: LOIC REMY ASHEREHEKEA KUTUA CHELSEA KWA KUIPIGIA BAO LA USHINDI UFARANSA DHIDI YA HISPANIA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top