• HABARI MPYA

    Saturday, September 13, 2014

    DIEGO 'MABAO' COSTA APIGA TATU PEKE YAKE CHELSEA IKIUA 4-2 ENGLAND, REMY NAYE ATUPIA

    MSHAMBULIAJI Diego Costa ameendeleza mwanzo mzuri katika Ligi Kuu ya England baada ya kuifungia Cheslea mabao matatu peke yake katika ushindi wa 4-2 dhidi ya Swansea City Uwanja wa Stamford Bridge, Londo.
    Wakati mchezaji huyo bora wa Agosti, akipiga hat trick yake ya kwanza England na kufikisha mabao saba ndani ya mechi nne, bao lingine la Chelsea lilifungwa na mchezaji mpya, Loic Remy aliyeingia kuchukua nafasi ya Coasta kipindi cha pili. Beki John Terry alijifunga kuipatia Swansea ambayo bao lake lingine lilifungwa na Jonjo Shelvey.
    Kuna maswali? Diego Costa amepiga hat trick Chelsea ikiua 4-2 Ligi Kuu England

    Kikosi cha Chelsea kilikuwa; Courtois, Ivanovic, Cahill, Terry, Azpilicueta, Matic, Fabregas/Salah dk82, Schurrle/Ramires dk46, Oscar, Hazard na Diego Costa/Remy dk72.
    Swansea: Fabianski, Rangel, Amat/Fernandez dk46, Williams, Taylor, Ki, Shelvey, Sigurdsson, Dyer, Routledge/Montero dk66 na Gomis/Bony dk76.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: DIEGO 'MABAO' COSTA APIGA TATU PEKE YAKE CHELSEA IKIUA 4-2 ENGLAND, REMY NAYE ATUPIA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top