Na Renatus Mahima, DAR ES SALAAM
UONGOZI wa Benki ya CRDB umesema mfumo wa tiketi za elektroniki uko tayari kutumika kwenye viwanja vilivyoidhinishwa kwa mechi za Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL).
Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), lililazimika kuzuia matumizi ya tiketi za mfumo huo msimu uliopita wa VPL kwa madai kuwa kulitokea tatizo la usalama wa mashabiki kwenye baadhi ya viwanja.
Mkurugenzi Mtendaji wa CRDB, Charles Kimei ameiambia BIN ZUBEIRY jijini Dar es Salaam kuwa mfumo huo uko tayari kutumika baada ya kurekebisha kasoro zilizojitokeza awali.
Kimei, ambaye ni daktari wa uchumi, alisema benki hiyo imefanya majaribio ya mfumo huo kwenye viwanja vya Kaitaba mjini Bukoba, Mkwakani jijini Tanga, Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro na Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya na kujiridhisha kwamba mfumo huo utafanya kazi bila matatizo msimu huu.
“Tumeongeza milango kwenye baadhi ya viwanja vilivyoleta matatizo msimu uliopita. Kwa sasa tunasubiri tamko la wenzetu wa TFF ili tusimike mfumo huo kwenye viwanja kama vile CCM Kambarage mjini Shinyanga na Nangwanda mjini Mtwara ambako haujasimikwa,” alisema Kimei.
Uwanja wa CCM Kambarage unatumiwa na timu ya Stand United kama uwanja wa nyumbani huku Ndanda FC ikiutumia Uwanja wa Nangwanda kama wao wa nyumbani, timu hizo mbili zimepanda Ligi Kuu msimu huu.
Alivitaja viwanja ambavyo viko tayari kwa mfumo huo msimu huu ni pamoja na Uwanja wa Chamazi, Taifa, Mkwakwani, Kaitaba, Jamhuri Morogoro na Sokoine Mbeya.
Viwanja vingine ambavyo viko tayari ni Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza na Uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha ambavyo hata hivyo, viko katika mikoa ambayo haina timu za Ligi Kuu, hivyo mfumo huo utatumika kwa mechi za Ligi Daraja la Kwanza Tanzania Bara (FDL).
Kwa mujibu wa Silas Mwakibinga, Ofisa Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi Kuu (TPLB), mfumo wa tiketi za elektroniki umechelewa kusimikwa kwenye baadhi ya viwanja vikiwamo CCM Kambarage na Nangwanda kwa sababu hapakuwa na timu za Ligi Kuu katika mikoa husika.
Juni mwaka huu serikali ilitoa sharti kwa TFF kuhakikisha mfumo wa tiketi za elektroniki unatumika katika mechi zote za soka zinazochezwa nchini ili kuzuia hujuma za mapato ya milangoni.
Akiwasilisha taarifa ya Kamati ya Bunge ya Uchumi, Viwanda na Biashara kuhusu utelezaji wa majukumu ya Wizara ya Fedha na Uchumi kwa mwaka wa fedha 2014/15 Bungeni mjini Dodoma Juni 4, mwaka huu, mwenyekiti wa kamati hiyo, Luhaga Mpina aliitaka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kutoa sharti kwa TFF kutumia mfumo wa tiketi za elektroniki ili kuongeza mapato ya nchi.
"Kamati inashauri TRA iweke sharti la lazima la kuitaka TFF kutumia mfumo wa tiketi za kielektroniki katika kuuza tiketi zake ikiwa ni jitihada za kuongeza mapato ya serikali," alisema Mpina.
Mbunge huyo wa Kisesa (CCM), alisema kwa muda mrefu serikali imekuwa haipati mapato ya kutosha kutoka katika sekta ya michezo hususan mpira wa miguu ulio chini ya TFF kutokana na mfumo dhaifu wa ukusanyaji fedha kipindi cha kuuza tiketi.
Mwaka juzi TFF ilitangaza zabuni ya kutengeneza tiketi za kielektroniki kwa ajili ya mechi za klabu na timu za taifa na benki ya CRDB ndiyo iliyoshinda tenda hiyo.
Kutangazwa kwa zabuni hiyo kulitokana na ripoti ya Mei 2011 ya Kamati Maalum ya Kudhibiti na Kuboresha Mapato ya TFF iliyopendekeza kuachwa mara moja kutumika kwa mfumo wa sasa wa tiketi za kawaida na kuanza kutumika tiketi za elektroniki.
Ukurasa wa 29 wa ripoti hiyo yenye jumla ya kurasa 95 na viambatanisho tisa, unasema: “Baadhi ya watendaji wakuu ndani ya TFF wanajihusisha na kuhujumu mapato kwa kuchapisha tiketi za ziada na kuziuza kwanza.”
“Kuna tiketi nyingi za kughushi/ bandia zinazotengenezwa kwa ushirikiano kati ya viongozi wa soka na wapenzi wa mpira wa miguu... TFF iache mara moja matumizi ya tiketi za kawaida na kuanza kutumia tiketi za kielektroniki,” inaeleza zaidi ripoti hiyo katika ukurasa wa 30.

.png)
0 comments:
Post a Comment