Micho Lugogo jana |
Na Mahmoud Zubeiry,
Kampala
KOCHA wa
Rwanda, Mserbia Milutin Sredojevic ‘Micho’ ameonyesha dalili za kutosha kwamba
anaiogopa Tanzania Bara kuelekea mchezo wa Robo Fainali, Kombe la Mataifa ya
Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Tusker Challenge kesho Uwanja wa Lugogo mjini
hapa.
Akizungumza
baada ya mechi ya jana, Micho alisema kwamba kuelekea mchezo wa kesho Tanzania
wana nafasi nzuri kwa sababu jana walikuwa mazoezini dhidi ya Somalia, wakati
Rwanda walikuwa wana mechi ngumu na Eritrea.
“Walikuwa
mazoezini tu na Somalia, wamepumzika zaidi, sisi tumecheza mechi ngumu, tena
napenda niseme dhidi ya timu ambayo imecheza soka ya kuvutia zaidi katika
mashindano haya. Nawapongeza (Eritrea) kwa hilo,”alisema Micho.
Pamoja na
hayo, Micho aliisifu timu yake kwamba daima katika mashindano haya huwa
haitolewi katika hatua ya makundi na jana imeendeleza utamaduni huo, baada ya
kufuzu Robo Fainali.
Micho
alisema anaiheshimu Tanzania ni timu nzuri na anatarajia mchezo utakuwa mgumu,
lakini watapigana kwa nguvu zao zote kuhakikisha wanashinda na kwenda Nusu Fainali.
Bara, Kilimanjaro
Stars itacheza na Rwanda katika Robo Fainali ya CECAFA Tusker Challenge kesho
kwenye Uwanja wa Lugogo kuanzia saa 8:00 mchana, wakati Zanzibar itacheza na
Burundi saa 10:00 jioni.
Robo Fainali
nyingine zitachezwa Jumanne Uwanja wa Mandela, Namboole, kati ya Kenya na
Malawi saa 10:00 jioni wakati wenyeji Uganda watacheza na Ethiopia saa 1:00
usiku.
Katika mechi
za jana, Bara iliilaza Burundi mabao 7-0 katika mchezo uliofanyika kwenye
Uwanja wa Lugogo mjini hapa. Matokeo hayo yanaifanya Bara itimize pointi sita
baada ya kucheza mechi tatu na sasa, wakishinda mbili na kufungwa moja.
Burundi
imemalizaa kileleni mwa Kundi B, kufuatia ushindi wa 1-0 dhidi ya Sudan, bao
pekee la Chris Nduwarugira jana.
Rwanda iliifunga
Eritrea 2-0, mabao ya Tadi Etikiama na Tumaine Ntamuhanga, huku Malawi ikiilaza
Zanzibar 2-0.
ROBO FAINALI
Desemba 3, 2012
Tanzania
Vs Rwanda Saa 8:00 mchana Lugogo
Zanzibar Vs Burundi Saa
10:00 jioni Lugogo
Desemba 4, 2012
Kenya Vs
Malawi Saa 10:00 jioni Namboole
Uganda Vs
Ethiopia Saa 1:00 usiku Namboole
VIWANGO VYA
UBORA FIFA
NCHI NAFASI
Uganda 86
Malawi 101
Ethiopia 102
Sudan 102
Rwanda 122
Burundi 128
Kenya 130
Tanzania 134
Zanzibar 134
Somalia 193
Eritrea 192
Sudan Kusini 200
(Viwango hivi vimetoka mwezi huu)