Haruna Niyonzima |
Na Mahmoud Zubeiry,
Kampala
NAHODHA wa
Rwanda, Haruna Niyonzima amesema anataka watu waondoe dhana kwamba wachezaji wa
Tanzania wanamjua vizuri yeye, hivyo watamdhibiti kwa urahisi katika mechi yake
ya kesho ya Robo Fainali, Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA
Tusker Challenge.
Rwanda
itamenyana na Tanzania Bara kesho kwenye Uwanja wa Lugogo katika Robo Fainali
ya Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Tusker Challenge.
Akizungumza
na BIN
ZUBEIRY jana, Niyonzima alisema kwamba kama wapo watu wanaamini yeye
hataidhuru Tanzania kwa sababu anacheza Ligi Kuu ya nchi hiyo, watakuwa
wanajidanganya.
“Kama wao
wananijua na watajifunza namna ya kunikaba, basi na mimi ninawajua na
nitajifunza namna yab kuwapita,”alisema kiungo huyo wa klabu ya Yanga SC ya Dar
es Salaam.
Niyozima
alisema anaiheshimu Tanzania Bara ni timu nzuri na ina wachezaji wazuri na
anaamini hata Kilimanjaro Stars pia wanaiheshimu Rwanda.
“Mchezo
utakuwa mgumu sana kwa kweli, lakini sisi hatuna hofu, tutapigana kwa uwezo
wetu wote ili tushinde,”alisema Niyonzima.