• HABARI MPYA

    Tuesday, May 08, 2012

    TWIGA STARS NA MADEMU WA ZIMBABWE JUMAMOSI TAIFA


    TIMU ya soka ya taifa ya wanawake, Twiga Stars itacheza na Zimbabwe katika mchezo wa kirafiki utakaofanyika Jumamosi wiki hii kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
    Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Boniphace Wambura Mgoyo ameiambia BIN ZUBEIRY leo mchana kwamba  
    Twiga Stars hivi iko katika ziara ya mechi za kirafiki katika mikoa ya Dodoma na Mwanza. Leo (Mei 8 mwaka huu) itacheza na kombaini ya Mkoa wa Dodoma ya vijana wenye umri chini ya miaka 17 katika mchezo utakaofanyika Uwanja wa Jamhuri, mjini Dodoma.
    Wambura amesema kesho (Mei 9 mwaka huu) itaondoka kwenda jijini Mwanza ambapo pia itacheza mechi moja ya kirafiki Mei 10 mwaka huu kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, na kurejea Dar es Salaam tayari kwa ajili ya mechi dhidi ya Zimbabwe.
    Amesema Zimbabwe inatarajia kuwasili kesho (Mei 9 mwaka huu) jioni kwa ndege ya South African Airways (SAA) ikiwa na msafara wa 25 na wataondoka Mei 14 mwaka huu alfajiri.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: TWIGA STARS NA MADEMU WA ZIMBABWE JUMAMOSI TAIFA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top