• HABARI MPYA

    Saturday, May 19, 2012

    RONALDO: MIMI NI BORA ZAIDI YA MESSI


    Ronaldo

    NYOTA wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo amesema kwamba amekataa kufananishwa na nyota wa BarcelonaLionel Messi kwa sababu wako tofauti, ingawa amesema hadi sasa amedhihirisha yeye ni bora zaidi ya mwenzake huyo.

    Mwanasoka huyo wa kimataifa wa Ureno, anaamini wachezaji wote yeye na mwenzake, wanafanya vizuri kadiri ya uwezo wao kuzisaidia klabu zao, ambayo inamsaidia kila mmoja kujipandisha hadhi.

    "Wakati fulani inanichosha," Ronaldo alisema akihojiwa na CNN World Sport. "Kwake pia, kwa sababu wanatulinganisha sisi wakati wote. Huwezi kulinganisha Ferrari na Porsche, kwea sababu ni injini tofauti. Huwezi kuzilinganisha. Anafanya mambo mazuri kwa Barcelona, nafanya mambo mazuri kwa Madrid, hivyo kila mmoja anasema, ni babu kubwa, kwake na kwangu, kwa sababu tunavunja rekodi zetu wenyewe, hivyo ni mambo adimu. 

    "Nafikiri tunasukumana wenyewe kwa wenyewe wakati fulani kwenye mashindano, hii ndio sababu ushindani ni mkubwa mno. Hii ndiyo kwa sababu Madrid na Barcelona ni timu bora duniani, kwa kila mmoja anamsukuma mwenzake. Si juu ya nani  ni mzuri. Sipendi kulinganishwa na mtu yeyote. Watu fulani wanasema mimi mzuri, wengine wanasema yeye, lakini mwisho wa siku, wanaamua nani ni mchezaji bora katika mashindano, ambaye nafikiri ni  mimi."

    Ronaldo amefunga mabao 46 katika La Liga msimu huu, wakati Messi amefunga 50 kwenye ligi hiyo Kuu Hispania na kutwaa kiatu cha dhahabu, maarufu kama Pichichi.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: RONALDO: MIMI NI BORA ZAIDI YA MESSI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top