• HABARI MPYA

    Thursday, May 03, 2012

    MISS UKONGA KUPATIKANA MEI 5


    Washiriki Miss ukonga 2012

    WAREMBO 14 wanataraji kupanda jukwaani Mei 5 mwaka huu, katika Ukumbi wa Wenge Garden ulipo Ukonga Mombasa, jijini Dar es Salaam kuwania taji la Redds Miss Ukonga 2012.
    Akizungumza na Blogu hii mratibu wa Shindano hilo Daudi Mambya amesema kuwa warembo wote hao 14 wapo tayari kwa kuchuana vikali siku hiyo na maandalizi kwaajili ya shindano hilo yanaenda vizuri.
    “Warembo wote wapo kamili na tayari wako na ari kubwa ya kushindana jumamosi hii, na hadi sasa hakuna mrembo ambaye anatatizo”, amesema Mambya.
    Aidha Mambya amesema awali warembo hao ilikuwa wachujwe na kubaki 12 lakini kutokana na warembo wote kuwa na vigezo wameamua kuwaacha ili kuleta ushindani zaidi siku ya mashindano.
    Warembo hao ambao watapanda jukwaani kwa show kali na yaaina yake ya ufunguzi mwaka huu katika majukwaa ya Urembo nchini wataongozwa na Burudani kali kutoka kwa Mapacha 3.
    Mbali na kundi hilo la Mapacha 3 ambalo linawika Jijini Dar es Salaam kutokana na uhodari wao pia kutakuwepo na burudani nyingine za wasanii wa kizazi kipya.
    Mambya aliwataja warembo hao 14 watakao panda jukwaani kuwa ni Shekha Shally, Zainab Matagi, Mageshi Boniface, Juliana Henry, Mary Chizi, Leah John’s na Magdalena Gisse.
    Wengine watakao shiriki Redds Miss Ukonga 2012 ni pamoja na Zawadi Mwambe, Stellah Maurice, Amina Sangawe, Elizabeth Pertty, Alicia Donatus, Rachel Isaaack na Amina Ramadhani.
    Shindano la Miss Ukonga 2012 linadhaminiwa na Redds Primium Cold, Clouds FM, Father Kidevu Blog, Kiota Jungle, V Mask Logistic, Mambya Insurance, Mamushka Pub & Catering, Hill tech Resort, Mr Mabaga, G Obonyo na Excel Beaut Salon.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MISS UKONGA KUPATIKANA MEI 5 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top