TIMU ya Norway imeibuka na ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya Senegal katika mchezo wa Kundi I Fainali za Kombe la Dunia Alfajiri ya leo Uwanja wa MetLife, East Rutherford, New York, Marekani.
Mabao ya Norway yamefungwa na beki wa Torino ya Italia, Marcus Holmgren Pedersen dakika ya 43 na mshambuliaji wa Manchester City ya England, Erling Braut Haaland mawili, dakika ya 48 na 58.
Kwa upande wao, Senegal ‘Simba wa Teranga’ mabao yao yote yamefungwa na mshambuliaji wa Crystal Palaceya England, Ismaïla Sarr dakika ya 53 na 90’+3.
Mchezo uliotangulia wa Kundi I Ufaransa iliichapa Iraq 3-0, mabao ya Kylian Mbappé dakika ya 14 na 54 na Ousmane Dembélé dakika ya 66 usiku wa kuamkia leo Uwanja wa Lincoln Financial Field, Philadelphia, Pennsylvania nchini Marekani.
Msimamo wa Kundi I sasa Ufaransa inaongoza kwa pointi zake sita ikiizidi tu wastani wa mabao Norway, wakati Senegal na Iraq hazna pointi hata moja kufuatia mechi mbili mbili za mwanzo.


.png)
0 comments:
Post a Comment