• HABARI MPYA

    Tuesday, September 09, 2014

    WATURUKI WATAKA KUING'OA SAMSUNG KWENYE JEZI ZA CHELSEA

    SHIRIKA la ndege la Uturuki linawania kuchukua nafasi ya Samsung, ambao mkataba wao wa udhamini wa jezi za Chelsea unafikia tamati mwishoni mwa msimu.
    Shirika hilo la ndege la nne kwa ukubwa Ulaya, ambalo liliingia mikataba ya kukumbukwa na nyota kama Lionel Messi na Kobe Bryant, hive karibuni limekuwa wadhamini wa Barcelona, Manchester United na timu ya taifa ya Uturuki.
    Uzinduzi: Kocha wa Chelsea, Jose Mourinho (kushoto) na Mtendaji Mkuu, Peter Kenyon katika uzinduzi wa udhamini wa Sumsung mwaka 2005

    Samsung imekuwa mdhamini wa Chelsea tangu mwaka 2005 wakati Mtendaji Mkuu wa zamani, Peter Kenyon aliposema klabu hiyo inakwenda kuipaka dunia rangi ya bluu. 
    Chelsea ilisaini tena Mkataba wake na Samsung mwaka 2013, lakini ajabu haikutangazwa sana.
    Lucrative: Turkish Airlines have been a sponsor of Spanish giants Barcelona
    Shirika la ndege la Uturuki limekuwa wadhamini wa Barcelona
    Stars: Europe's fourth biggest airliner made a memorable commercial deal with Lionel Messi and Kobe Bryant
    Nyota: Shirika la nne la ndege kwa ukubwa Ulaya lilting Mkataba na Lionel Messi na Kobe Bryant
    Spreading their wings: Turkish Airlines linked up with Manchester United
    Shirika la Ndege la Uturuki pia lina uhusiano na Manchester United

    Chelsea ilikubali Mkataba wa miaka 10 wa vifaa vya michezo wenye thamani ya Pauni Milioni 300 na adidas msimu uliopita. 
    Pamoja na hayo, kiwango kinaonyesha ni jinsi gani Chelsea iko nyuma ya Manchester United katika masuala ya kibiashara. 
    Mkataba wa timu ya Old Trafford wa vifaa vya michezo na Chevrolet, ambao klabu hiyo iliupata miaka miwili kabla ya kuanza kwake msimu wa 2014-15, una thamani ya Pauni Milioni 50 kwa msimu. 
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: WATURUKI WATAKA KUING'OA SAMSUNG KWENYE JEZI ZA CHELSEA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top