• HABARI MPYA

    Tuesday, September 09, 2014

    UJUMBE WA BALOTELLI KWA WANAFUNZI WOTE DUNIANI, JAMAA KUMBE 'MCHARUKO' TU, LAKINI KICHWANI ZIMO

    PAMOJA na kuonekana kama mchezaji mtukutu uwanjani, lakini Mario Baloteli ameonyesha ni mtu anayejali masuala ya elimu baada ya kuposti ujumbe mzuri wa kuwatakia kila la heri wanafunzi wakirejea shuleni wiki hii.
    Mshambuliaji huyo wa Liverpool ameandika kwenye akaunti yake ya Instagram ujumbe usemao: "Hi watoto, leo mnaanza shule kwenye nchi nyingi. Ni kama mwanzo wa msimu kwenye soka. Huo ni wakati wa kufanya vizuri ili kujenga mustakabali mzuri wa maisha yako. Kila la heri!'
    Ujumbe huo ameuambatanisha na video fupi, amnayo mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24 aliyewahi kuchezea pia Manchester City, Inter Milan na AC Milan amesema: "Soma kwa vidii na chez a kwa bidii, nawatakia watoto wote kila la heri katika siku yako ya kwanza shule,".
    Super Mario: Balotelli amewaandikia ujumbe mzuri watoto wakirejea shule wiki hii
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: UJUMBE WA BALOTELLI KWA WANAFUNZI WOTE DUNIANI, JAMAA KUMBE 'MCHARUKO' TU, LAKINI KICHWANI ZIMO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top