GWIJI wa Manchester United, Paul Scholes haoni namna gani kocha Louis van Gaal ataweza kuwatumia kwa pamoja washambuliaji Wayne Rooney, Robin van Persie na Radamel Falcao katika kikosi kimoja.
Scholes anaamini kwamba Falcao, ambaye amesajiliwa kwa mkopo kutoka Monaco katika siku ya mwisho ya kufunga dirisha la usajili, ni mchezaji wa aina yake, lakini amesema klabu yake itaweza kuwatumia wawili tu kati ya washambuliaji wake hao watatu wenye majina makubwa.
Katika makala yake kwenye safu yake ya gazeti la The Independent, Scholes amesema: "Nilipomuona Falcao anachezea Porto, Atletico Madrid na Monaco, niliona mshambuliaji mzuri na mwenye rekodi ya kufunga mabao, ambayo ipo wazi katika dunia hii,".
Nani atasugua benchi? Paul Scholes haoni namna gani Louis van Gaal atapanga washambuliaji wake watatu kwa pamoja uwanjani
Wapi atafaa? Radamel Falcao akiwa na Ryan Giggs baada ya kusaini kwa mkopo
"Falcao analeta ushindani katika safu ya ushambuliaji ya United. Hakuna namna ambayo Van Gaal anaweza kuwachezesha Rooney, Van Persie na Falcao pamoja. Itakuwa wawili kati yao, na akina mani hao wawili, ngumu kusema bado,".
Scholes anaamini usajili uliofanywa na klabu hiyo dirisha hili, ambao imeshuhudiwa wachezaji Luke Shaw, Ander Herrera, Marco Rojo, Angel di Maria na Danny Blind wakitua Old Trafford wote wakiigharimu United Pauni Milioni 150, umempatia Van Gaal kikosi cha kumaliza ndani ya nne bora kwenye Ligi Kuu ya England.
"Sifikiri kama kuna uwezo wa kubeba taji la ubingwa wa ligi, lakini nafasi ya kucheza Ligi ya Mabingwa Ulaya ndiyo lengo. Sasa, ni juu yake Van Gaal kuisuka timu.
Licha ya kuvutiwa na wachezaji wapya waliosajiliwa, Scholes amesema amesikitishwa kuona kijana aliyeibuliwa kutoka akademi, Danny Welbeck akiuzwa kwa Pauni Milioni 16 Arsenal - hata kama hawezi kufunga mabao 20 kwa msimu.
"Imeonyesha thamani yake Danny kwa klabu kubwa kama Arsenal kumsajili. Atakuwa usajili mzuri kwa Arsene Wenger,"amesema. Danny hawezi kufunga mabao 20 hadi 25 msimu mmoja, lakini anaweza kuifungia Arsenal mabao 10 hadi 15,".



.png)
0 comments:
Post a Comment