MSHAMBULIAJI Daniel Sturridge yuko shakani kuichezea England dhidi ya Uswisi baada ya kuumia mazoezini leo.
Kikosi cha Roy Hodgson kinaanza kampeni yake ya kuwania kufuzu kwenye michuano Euro mjini Basle Jumatatu dhidi ya timu ambayo inashika nafasi ya tisa kwa ubora duniani.
Ni mechi ambayo huenda wakamkosa Sturridge baada ya mpachika mabao huyo kuumia mazoezini Uwanja wa St George's Park asubuhi ya leo.
Taarifa katika akaunti ya Twitter ya England imesema; "Daniel Sturridge ameumia asubuhi hii na atakwenda kufanyiwa vipimo mchana huu. Kisha atatazamwa na matabibu wa England,".
Kukosekana kwa Sturridge kutafanya mchezaji mwenzake wa Liverpool acheze namba 10 pamoja na Nahodha Wayne Rooney katika safu ya ushambuliaji.
Gary Cahill alikuwa mchezaji pekee anayekosekana kwenye kikosi cha England kinachoendelea na maandalizi Uwanja wa St George's Park baada ya beki huyo wa Chelsea kuumia enka katika ushindi wa 1-0 dhidi ya Norway Jumatani.
Hodgson anatarajia Cahill atarejea kikosini Jumamosi na kuwa fiti kucheza dhidi ya Uswisi baada ya kuwa tayari amewapoteza wachezaji wawili kati ya 22 wa kikosi chake halisi kwa sababu kuumia.
Jack Colback amerejea Newcastle baada ya kushindwa kupona enka aliyoumia dhidi ya Crystal Palace, na Ben Foster amejitoa kwa maumivu ya kidole gumba.
Taarifa kwenye akaunti ya Tweeter ya England ikithibitisha kuumia kwa mshambuliaji wa Liverpool
0 comments:
Post a Comment