• HABARI MPYA

    Thursday, September 11, 2014

    MAYWEATHER: NAZEEKA, LAKINI SHUGHULI BADO IMO MTAONA JUMAMOSI

    BONDIA Floyd Mayweather amesema kwamba umri umeenda sasa na anakaribia miaka 40, lakini bado ana uwezo mkubwa ambao atauonyesha Jumamosi mjini Las Vegas katika pambano la marudiano dhidi ya Marcos Maidana.
    Wawili hao walizipiga awali Mei mwaka huu, wakati Mayweather aliposhinda kwa utata na kuendeleza rekodi yake ya kutopoteza pambano baada ya kupanda ulingoni mara 46.
    Mayweather, mwenye umri wa miaka 37, amebakiza mapambano kadhaa kabla ya kustaafu, lakini amesema hakuna jinsi angekwepa kupambana na mkali wa Argentina, Maidana kwa mara ya pili baada ya watu kuomba sana pambano la marudiano baina yao.

    Floyd Mayweather Jr na Marcos Maidana wakitambiana wakati wa mkutano na Waandishi wa Habari ukumbi wa MGM Grand Hotel

    "Ninafahamu ninakaribia miaka 40, lakini bado nina nguvu," amesema Mayweather. "Bado ninajisikia vizuri na ninataka kwenda huko kupambana. Ninakwenda kuwapa nyinyi watu kile mnachotaka kuona.
    "Pambano la kwanza lilikuwa tamu tamu sana. Natumai pambano la safari hii pia litakuwa lenye mvuto zaidi," amesema. 
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MAYWEATHER: NAZEEKA, LAKINI SHUGHULI BADO IMO MTAONA JUMAMOSI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top