Na Mwandishi Wetu, SONGEA
KLABU bingwa ya zamani Tanzania, Majimaji FC ya Songea mkoani Ruvuma imetaja kikosi cha wachezaji 26 iliyowasajili kwa ajili ya Ligi Daraja la Kwanza Tanzania Bara msimu wa 2014-2015.
Ofisa Habari wa Majimaji, Nathan Mtega ameiambia BIN ZUBEIRY katika taarifa yake ya leo kwamba, kikosi hicho kitaingia kambini muda wowote kuanzia sasa.
Amesema katika kikosi hicho, wachezaji 12 ni wapya ambao ni Oswald Issa, Samir Said, Emmanuel Maganga, Ally Mohamed, Kudra Omary, Said Fundikira, Mrisho Said, Idd Kipagule, Mohamed Omary, Yohana Kimburu na Msafiri Abdallah.
Amewataja wachezaji wa zamani 14 watakaoendelea kuitumikia klabu hiyo kuwa ni pamoja na Anthony Mwingira, Eliuta Ndunguru, Bahati Yussuf, Gerarrd Mbena, Abdallah Aus, Ditram Nchimbi, Filoteus Mahundi, Mpoki Mwakinyuke, Alex Zegega, Sadiq Gawaza, Odo Nombo, Frank Sekule, Marcel Boniventure na Freddy Mbuna.
“Wachezaji hao wote taratibu za usajili wao zimekamilika na uongozi wa klabu unatoa tahadhari kwa klabu ambazo zimeingia mikataba na baadhi ya wachezaji wa Majimaji, kuwa kufanya hivyo ni kukiuka kanuni na taratibu za soka. Klabu haitakaa kimya, kwa sababu wachezaji wote wa Majimaji wana mikataba ya kisheria na klabu,”amesema Mtega.

![]() |
Ofisa Habari wa Majimaji ya Songea, Nathan Mtega ametaja kikosi cha msimu ujao |
Amewataja wachezaji wa zamani 14 watakaoendelea kuitumikia klabu hiyo kuwa ni pamoja na Anthony Mwingira, Eliuta Ndunguru, Bahati Yussuf, Gerarrd Mbena, Abdallah Aus, Ditram Nchimbi, Filoteus Mahundi, Mpoki Mwakinyuke, Alex Zegega, Sadiq Gawaza, Odo Nombo, Frank Sekule, Marcel Boniventure na Freddy Mbuna.
“Wachezaji hao wote taratibu za usajili wao zimekamilika na uongozi wa klabu unatoa tahadhari kwa klabu ambazo zimeingia mikataba na baadhi ya wachezaji wa Majimaji, kuwa kufanya hivyo ni kukiuka kanuni na taratibu za soka. Klabu haitakaa kimya, kwa sababu wachezaji wote wa Majimaji wana mikataba ya kisheria na klabu,”amesema Mtega.
0 comments:
Post a Comment